Mashambulizi hayo ni pamoja na shambulizi lililofanyika katika mji wa Beit Lahiya, kaskazini mwa Gaza, ambalo liliua watu 10, madaktari wamesema.
Mashambulizi mengine ya Israel yalilenga eneo la Katikati mwa Gaza na Rafah kusini mwa Palestina.
Ghasia hizo zimetokea wakati kukiwa na juhudi mpya za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas ambayo yatajumuisha kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa na wanamgambo hao huko Gaza.
Maafisa wa Israel walisema katika siku za hivi karibuni wana matumaini ya kufikia hatua katika mazungumzo ya muda mrefu yaliyokwama, huku Hamas ikisema Jumanne inaamini makubaliano yanawezekana ikiwa Israel haitaleta masharti mapya.
Forum