Vyama vya mrengo wa kulia vilifanikiwa kupata karibu robo ya kura kote barani humo kwenye uchaguzi wa wabunge wa Umoja wa Ulaya wa mwezi Juni, ingawa vyama vya mrengo wa kati vimeendelea kushikilia madaraka kwenye taasisi za EU mjini Brussels.
Nchini Ufaransa chama cha Marine Le Pen, cha National Rally kilishinda kwa idadi kubwa ya kura za Ufaransa kwenye uchaguzi wa bunge la EU, kikijipatia asilimia 31. Chama cha rais wa Ufaransa Emmanuel Macron cha Renaissance, kilipata asilimia 15 tu ya kura, na kupelekea kuvunjwa kwa bunge na kuitishwa kwa uchaguzi mkuu, hatua inayotoa nafasi kwa chama cha National Rally kuunda serikali kwa mara ya kwanza.
“Tuko tayari kuongoza iwapo watu wa Ufaransa watatuunga mkono kwenye uchaguzi wa bunge ujao,” La Pen aliwaambia wafuasi wake. “Tupo tayari kubadili mambo na kulinda maslahi ya watu wa Ufaransa, pamoja na kusitisha wimbi la wahamiaji,” alisema. Hata hivyo vyama vya mrengo wa kushoto kati vimeunda muungano unaolenga kukizuia chama cha National Rally kuchukua madaraka.
Forum