Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 19:48

Nyaya za internet zilizoharibiwa chini ya Bahari ya Baltic zarekebishwa


Meli ya mizigo ya China ya Yi Peng 3, inayoshukiwa kuharibu nyanya za internet chini ya bahari ya Baltic.Reuters
Meli ya mizigo ya China ya Yi Peng 3, inayoshukiwa kuharibu nyanya za internet chini ya bahari ya Baltic.Reuters

Moja ya nyaya za kupeleka internet chini ya bahari ya Baltic anayoshukiwa kuharibiwa maksudi mapema mwezi huu imekarabatiwa kulingana na msemaji wa kampuni husika ya Arelion.

Ukarabati wa nyaya hizo zinazounganisha Sweden na Lithuania ulikamilika Alhamisi na mfumo huo umeanza kufanya kazi kikamilifu, msemaji huyo kwa jina la Martin Sjogren ameongeza kusema.

Nyanya zingine mbili za aina hiyo zinazounganisha Finland na Ujerumani ziliharibiwa chini ya saa 24 kati ya Novemba 17-18, na kupelekea waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius kusema kuwa wanashuku ziliharibiwa maksudi. Nyaya za chini ya bahari husafirisha data ya internet kote ulimwenguni na ni kiungo muhimu kwa kuwa zinaunganisha mawasiliano kati ya nchi.

Wachunguzi wanashuku kwamba ziliharibiwa na meli kubwa ya mizigo cha China ya Yi Peng 3, wakati waziri mkuu wa Sweden Ulf Kristersson akisema kuwa nchi yake imetuma ombi rasmi kwa China la ushirikiano kuhusu kilichopelekea uharibifu huo chini ya maji ya bahari ya Baltic. Msemaji wa kampuni iliofanya ukarabati Martin Sjogren amesema kuwa wanashirikiana na polisi wa Sweden kwenye uchunguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG