Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 19:09

Tuzo za Haki za Binadamu za mwaka 2024 zatolewa Washington


Rufat Safarov, mtetezi wa haki za binadamu wa Azerbaijan aliyezuiliwa kusafiri Marekani ili kupokea tuzo yake.
Rufat Safarov, mtetezi wa haki za binadamu wa Azerbaijan aliyezuiliwa kusafiri Marekani ili kupokea tuzo yake.

Rufat Safarov, mwanaharakati maarufu wa kutetea haki za binadamu kutoka Azerbaijan, ni miongoni wa watu waliopokea tuzo za mwaka huu za Mtetezi wa Haki za Binadamu, kutoka wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini Washington.

Hata hivyo hakuweza kuhudhuria hafla hiyo ya Jumanne kwa kuwa alikamatwa Desemba 3, saa chache baada ya kuutembelea ubalozi wa Marekani mjini Baku, ili kuomba visa ya kuja Marekani.

Wakati wa hafla hiyo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alionyesha kiti kitupu kilichotengwa kwa ajili ya Safarov, wakati akiomba kuachiliwa kwake mara moja. “Kama muonavyo, kiti kimoja kwenye jukwaa hili ni kitupu. Ni cha Rufat Safarov, mtetezi wa haki za binadamu kutoka Azerbaijan, ambaye nimemzungumzia muda mfupi uliopita,” Blinken alisema.

Watu wengine waliopokea tuzo hizo ni kutoka Bolivia, Columbia, Eswatini, Ghana, Kuwait, Myanmar na Kyrgyzstan, ambao walipiga picha pamoja na Blinken. Jumatano, waziri huo ametoa wito mwingine kwa serikali ya Azerbaijan wa kumuachiliwa kwa Safarov pamoja na watu wengine wanaozuiliwa kutokana na harakati zao za kutetea haki za binadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG