Katibu mkuu wa Umoja huo amesema janga la kibinadamu la Afghanistan ni la pili baya zaidi duniani baada ya Sudan. Tom Fletcher ambaye ni naibu katibu mkuu wa UN wa masuala ya kibinadamu na dharura, amekiambia kikao cha robo mwaka cha Baraza la Usalama kwamba pendekezo hilo huenda likawa na athari za kudumu kwenye huduma za afya kwa wanawake na wasichana wa Afghanistan.
Mapema mwezi huu, utawala wa Taliban uliamuru vyuo vya umma na binafsi vya kutoa mafunzo ya utabibu visitishe mara moja kuandikisha wanafunzi wanawake pamoja na kuwazuia kumaliza mitihani yao ya mwisho wa muhula. Hata hivyo amri hiyo ya ghafla ilitoa muda wa siku kumi kwa vyuo hivyo kuwaruhusu wanafunzi wa kike kufanya mitihani ya muhula.
Sekta ya afya ndiyo pekee iliyokuwa imebaki kwa wanawake wa Afghanistan kupata elimu ya juu kufuatia kupigwa marufuku kwa elimu ya juu ya wanawake na serikali hapo nyuma, amesema Fletcher. Amesema kuwa hatua hiyo itaathiri zaidi ya wakunga 36,000 pamoja na wauguzi 2,800 waliokuwa kwenye sekta ya ajira katika miaka michache ijayo, na viwango vya vifo vya watoto huenda vikaongezeka, vifo vya wajawazito pamoja na akina mama nchini humo.
Forum