Wakati wa ziara ya Rais wa Marekani Joe Biden mapema mwezi ujao nchini Angola, ataangazia mradi wake mkubwa wa kimiundomsingi, unaolenga kuunganisha usafirishaji wa bidhaa barani Afrika.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema Jumatano kwamba atamteua Luteni Jenerali mstaafu wa jeshi Keith Kellog kuwa msaidizi wake na mjumbe maalum kwa ajili ya Ukraine na Russia.
Sitisho la mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah lenye makao yake nchini Lebanon lilianza kutekelezwa mapema Jumatano na hivyo kusimamisha mapigano ambayo viongozi wa Marekani na Ufaransa walisema yanaweza kufungua njia ya kuelekea kwenye sitisho jingine huko ukanda wa Gaza.
Idara ya polisi wa kimataifa ya Interpol imesema Jumanne kwamba imekamata zaidi ya washukiwa 1,000 wa uhalifu wa kimitandao barani Afrika, wakati wa operesheni iliyochukua miezi miwili.
Israel Jumanne jioni imekubali kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah la Lebanon, hatua ambayo huenda ikamaliza vita vilivyodumu kwa mwaka mmoja, iwapo sitisho hilo litaanza kutekelezwa Jumatano.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu alianza mkondo wa mwisho wa msimu wa sherehe akiwa madarakani kweye White House kwa kutoa msamaha kwa bata mzinga wawili ambao hawatachinjwa wakati wa Sikukuu ya Kutoa Shukurani mwishoni mwa wiki, wakiwa kusini mwa jimbo la Minnesota.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameondolewa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili, wakati akielekea kuapishwa kama rais wa 47 wa Marekani Januari 20.
Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Zambia wameelezea wasiwasi wao kutokana na ongezeko la ukamataji na kuzuiliwa kwa muda mrefu kwa viongozi wa upinzani.
Wapiga kura nchini Gabon walielekea kwenye vituo vya kupigia kura siku ya Jumamosi ili kuamua kuhusu katiba mpya ambayo huenda ikafungua njia ya utawala wa kidemokrasia baada ya mapinduzi yaliyouondoa madarakani utawala wa familia ya Bongo mwaka jana.
Mkuu wa ofisi ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa Jumamosi aliyasihi mataifa ya G20 kushinikiza kuendelea kwa mazungumzo ya COP29 kuelekea makubaliano ya kuongeza fedha kwa ajili ya nchi zinazoendelea, akionya kuwa bado kuna "njia ndefu ya kwenda" katika suala hilo.
China imeongeza juhudi za kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Ulaya baada ya uchaguzi wa Marekani, wakati maafisa wake wa ngazi ya juu, pamoja na vyombo vya habari wakisema kuwa hatua hiyo itakuwa na manufaa kwa Beijing na Brussels.
Idhaa ya Uajemi ya Sauti ya Amerika Alhamisi imeelezea kushtushwa na pia kuomboleza kufuatia kujiua kwa mmoja wa wafanyakazi wao wa zamani ambaye aliruka kutoka kwa jumba la ghorofa mjini Tehran, kama ishara ya kupinga utawala kandamizi wa Iran.
Upigaji kura wa Rais kwenye eno lililojitenga na Somalia la Somaliland umekamilika Jumatano bila matatizo yoyote.
Kushuka kwa vifo kutokana na utumizi kupita kiasi wa dawa za kulevya hapa Marekani mwaka huu kumetoa matumaini kwa wataalam kwamba hatua muhimu zimepigwa katika kupambana na janga hilo.
Rais-mteule wa Marekani, Donald Trump Jumatano alikwenda White House kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne kukutana na Rais anayeondoka mamlakani Joe Biden.
Marekani imesema Jumanne kuwa Israel imepiga hatua za kuwezesha upelekaji wa misaada huko Gaza kama Washington ilivyoomba, ikiwa na maana kwamba utawala wa Biden utaendelea kutoa silaha kwa Israel.
Mamlaka ya kitaifa ya kusimamia safari za ndege hapa Marekani Jumanne imetangaza kuwa itapiga marufuku safari za ndege za Marekani kuelekea Haiti kwa siku 30 kufuatia kushambuliwa kwa risasi kwa ndege ya shirika la Spirit Airlines na magenge yenye silaha.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump, kwa haraka anajaza utawala wake mpya na maafisa wa Repablikan, ambao wamekuwa waaminifu zaidi kwake kisiasa katika miaka minne tangu aondoke madarakani.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Thomas Homan, ambaye alikuwa kaimu mkuu wa uhamiaji kwenye muhula wake wa kwanza, kama mkuu wa uhamiaji kwenye serikali yake mpya.
Mwanahabari wa Sweden mwenye asili ya Eritrea ambaye amekuwa kizuizini Eritrea bila mawasiliano kwa zaidi ya miaka 23 Jumatatu amepewa tuzo ya Sweden ya Haki za binadamu kutokana na juhudi zake za kupigania haki ya kijieleza, jopo la tuzo hiyo limesema.
Pandisha zaidi