Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 08:11

Marekani yapongeza juhudi za Israel za upelekaji misaada Gaza


Lori lililobeba misaada kuelekea Ukanda wa Gaza kwenye mpaka wa Kerem Shalom kusini mwa Israel, Nov. 11, 2024.
Lori lililobeba misaada kuelekea Ukanda wa Gaza kwenye mpaka wa Kerem Shalom kusini mwa Israel, Nov. 11, 2024.

Marekani imesema Jumanne kuwa Israel imepiga hatua za kuwezesha upelekaji wa misaada huko Gaza kama Washington ilivyoomba, ikiwa na maana kwamba utawala wa Biden utaendelea kutoa silaha kwa Israel.

Naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Vedant Patel ameambia wanahabari kwamba “ Kufikia sasa hatujafanya tathmini yoyote inayoashiria kuwa Israel imevunja sheria za Marekani.” Marekani Oktoba 13 iliambia Israel kwamba ilikuwa na muda mwa mwezi mmoja wa kuongeza upelekaji wa misaada huko Gaza ambako miezi 13 ya vita kati ya Israel na kundi la Hamas vimesababisha janga la kibinadamu.

Iwapo Israel haingefanya hivyo kufikia Jumanne, basi Marekani ingepunguza upelekaji wa silaha kwake. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Jumatatu alikutana na mshauri mkuu wa kiusalama wa kitaifa wa Israel Ron Dermer mjini Washington, ili kutathmini hatua zilizopigwa na Israel kuelekea upelekaji wa misaada huko Gaza.

Mjumbe wa Marekani kwenye UN Linda Thomas-Greenfield ameambia Baraza la Usalama la Umoja huo kwamba Israel imepiga hatua muhimu zikiwemo kurejesha upelekaji wa misaada kaskazini mwa Gaza, lakini ni lazima ihakikishe kuwa inatimiza majukumu yake yote kadri muda unavyokwenda.

Forum

XS
SM
MD
LG