Baraza la mpito la Haiti, ambalo liliundwa ili kurejesha mfumo wa demokrasia nchini humo, Jumapili limetia saini amri ya kiutendaji ya kumfuta kazi kaimu waziri mkuu Garry Conille, na kuteuwa mfanyabiasha Alix Didier Fils-Aime, ambaye awali aliitaka kazi hiyo, kuchukua nafasi yake.