Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 09, 2024 Local time: 03:21

Korea Kaskazini na Russia zafanya mazungumzo Moscow


Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov akimkaribisha mwenzake wa Korea Kaskazini Choe Son Hui, Moscow, Russia, Novemba 1, 2024. Russian Foreign Ministry/Handout via REUTERS
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov akimkaribisha mwenzake wa Korea Kaskazini Choe Son Hui, Moscow, Russia, Novemba 1, 2024. Russian Foreign Ministry/Handout via REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui, amewasili Moscow kwa mazungumzo na mwenzake wa Russia Sergei Lavrov Ijumaa.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova, amechapisha kwenye ukurasa wake wa Telegram, picha za mawaziri hao wawili wakiwa kwenye kituo cha treni, mjini Moscow.

Maria Zakharova
Maria Zakharova

Zakharova amesema kwamba mazungumzo ya leo kati ya viongozi wa Russia na Korea kaskazini yatafanyika mjini Moscow.

Ziara ya Choe ambayo ni ya pili katika muda wa wiki sita, inajiri baada ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora yake ya masafa marefu wiki hii na Washington kusema kwamba Korea kaskazini imetuma wanajeshi 10,000 nchini Russia, ikiwemo 8,000 katika eneo la Kursk la Russia ambalo wanajeshi wa Ukraine wameingia.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema kwamba Marekani inatarajiwa wanajeshi wa Korea kaskazaini walio Kursk, kuanza kupigana dhidi ya wanajeshi wa Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG