Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 07, 2024 Local time: 00:16

Putin anasema Moscow itatumia majibu tofauti kama Ukraine itatumia silaha nzito


Rais wa Russia Vladimir Putin. Oct. 24, 2024.
Rais wa Russia Vladimir Putin. Oct. 24, 2024.

Rais wa Russia Vladimir Putin amesema Moscow itatumia majibu mbalimbali kama Marekani na washirika wake wa NATO watairuhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu za Magharibi kushambulia ndani ya Russia, kulingana na matamshi yaliyochapishwa leo Jumapili.

“Wizara ya ulinzi ya Russia inafikiria jinsi ya kujibu mashambulizi ya masafa marefu kwenye ardhi ya Russia, itatoa majibu mbalimbali”, Putin alimwambia mwandishi wa televisheni ya taifa, Pavel Zarubin katika matamshi ya video yaliyochapishwa kwenye mtandao wa Telegram kwenye akaunti ya Zarubin.

Wakati huo huo, ulinzi wa anga wa Russia uliharibu au kuzuia ndege 51 zisizo na rubani za Ukraine usiku wa kuamkia Jumapili, wizara ya ulinzi ya Russia imesema mapema Jumapili. Ndege 18 kati ya hizo zilinaswa katika mkoa wa Tambov, takriban kilomita 450 kusini mashariki mwa Moscow, wizara hiyo imesema kwenye program ya Telegram katika ujumbe wa maandishi.

Ndege nyingine 16 ziliharibiwa katika mkoa wa mpakani wa Belgorod na katika mikoa mingine ya Voronezh, Oryol na Kursk kusini mwa Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG