Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 14:39

Ujerumani kufunga ubalozi wa Iran kufuatia kuuwawa kwa Sharmahd


Rais wa Ujerumani mwenye asili ya Ujerumani Jamshid Sharmahd, aliyeuwawa na Iran kwa tuhuma za kushambulia msikiti 2008.
Rais wa Ujerumani mwenye asili ya Ujerumani Jamshid Sharmahd, aliyeuwawa na Iran kwa tuhuma za kushambulia msikiti 2008.

Ujerumani Alhamisi imesema kuwa itafunga ubalozi wa Iran nchini humo yakiwa majibu ya tangazo la Iran la kuuwa Jamshid Sharmahd, mjerumani mwenye asili ya Iran, na aliyekuwa mkazi wa Marekani mapema wiki hii.

“Tumeweka bayana kwa Tehran kwamba mauaji ya raia ya wa Ujerumani yatakuwa na athari zake,” amesema waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock , wakati akitangaza kufungwa kwa balozi za Iran kwenye miji ya Frankfurt, Munich na Hamburg. Aliongeza kusema kuwa ubalozi wa Iran uliopo Berlin utabaki, na kwamba Ujerumani itaendelea na mahusiano ya kidiplomasia na Iran kupitia ubalozi wake mjini Tehran.

Baerbock alisema kuwa mauaji hayo ambayo yamefanyika wakati kukiwa na taharuki Mashariki ya Kati yanaonyesha kuwa utawala wa kidikteta wa Iran hauheshimu diplomasia ya kawaida. Sharmhad mwenye umri wa miaka 69 alituhumiwa kuhusika kwenye shambulizi baya la bomu kwenye msikiti mmoja mjini Shiraz, Iran mnamo 2008.

Alifunguliwa mashitaka ya ufisadi Duniani, neno ambalo hutumiwa na Iran kuelezea hatia baya kadhaa zikiwemo za ukiukaji wa maandili ya Kiislamu. Hata hivyo familia yake imekanusha madai dhidi yake. Kwenye mahojiano ya kipekee na VOA Idhaa ya Uajemi, binti ya Sharmhd, Ghazaleh Sharmahd amesema kuwa kuuwawa kwa baba yake Jumatatu hakutadumaza vuguvugu la kuitisha haki Iran. “Walifanya makosa kuuwa baba yangu wakifikiri kuwa vugu vugu la watu wa Iran litakoma,” alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG