Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 18:03

Mataifa 22 yapo kwenye hatari ya njaa duniani, UN yasema


Ardhi iliokauka kutokana na ukame Saudi Arabia.
Ardhi iliokauka kutokana na ukame Saudi Arabia.

Umoja wa Mataifa kupitia ripoti ya Alhamisi umesema kuwa ghasia, mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na changamoto za kiuchumi zimepelekea njaa na wakati mwingine hali ya ukame kwa mataifa 22 pamoja na maeneo, bila kuwa na dalili za hali kuimarika ndani ya miezi 6 ijayo.

Arif Husain, ambaye ni mchumi mkuu kwenye Shirika la Chakula Duniani WFP, amesema kuwa hali ni mbaya zaidi kwenye Ukanda wa Gaza, Sudan, Sudan Kusini, Haiti na Mali, ambako mamilioni ya watu wapo kwenye hatari zaidi ya ukosefu wa usalama wa chakula, ikiwa na maana kwamba hali ya njaa kuu unashuhudiwa.

Huko Gaza, mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa yameonya kuhusu kudorora kwa hali katika miezi ya karibuni. Hali hiyo imechochewa zaidi na mapigano ya vita vya miezi 13 kati ya Israel na kundi la Hamas ambavyo vimeifanya hatari kupeleka misaada ya kibinadamu pamoja misaada mingine kwa Wapalestina waliokwama kwenye vita hivyo.

Husain ameongeza kusema kuwa asilimia 91 ya wakazi wa Gaza wapo kwenye baa la njaa, takriban 345,000 miongoni mwao wakikabiliwa na hali zinazofanana na ukame. Hali ya Sudan ni mbaya zaidi kutokana na kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa ni kubwa zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG