Mashambulizi kadhaa yaliyolenga masanduku ya kubebea kura kote Marekani yameongeza shinikizo kwa maafisa wa majimbo na mitaa, wanaotarajia kuwepo kwa uchaguzi wa amani wa rais mwaka huu.
Muungano wa vyama unaoongoza Japan, Jumapili, umepoteza wingi wake kwenye uchaguzi wa kitaifa wa Jumapili, hali ambayo imezua wasi wasi kuhusu serikali mpya itakayoundwa kwenye taifa hilo la nne kiuchumi duniani.
Chama cha upinzani cha Lithuania cha Social Democrats, kilionekana kuongoza kwenye kura ya pili ya bunge Jumapili, wakati wapiga kura wakiashiria kuwa na wasi wasi kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, pamoja na tishio la kiusalama kutoka kwa Russia ambaye ni jirani.
Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani Alhamisi imetangaza kanuni mpya zinazotoa ulinzi wa muda kwa baadhi ya wahamiaji wa Lebanon waliopo Marekani, wakiruhusiwa kuendelea kuishi na kufanya kazi.
Taarifa ya Jumanne imesema kuwa Pakistan imekubali kuimarisha usalama wa raia wa China pamoja na miradi ya China iliyopo kwenye taifa hilo la Kusini mwa Asia, wakati Beijing ikiomba hatua za haraka za kiusalama kuchukuliwa, kufuatia kuongezeka kwa tishio kutoka kwa wanamgambo.
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema Jumanne kwamba limeweza kuendesha kampeni ya utoaji wa chanjo za polio katikati mwa Gaza kwa maelfu ya watoto licha ya mashambulizi ya Israel kwenye maeneo maalum yaliyotengwa saa chache kabla ya mashambulizi hayo.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy, hivi karibuni anatarajiwa kutembelea Beijing na Shanghai, ikiwa ziara ya ngazi ya juu zaidi nchini China tangu chama cha Labour kilipoingia madarakani.
Takriban waandamanaji 200 waliokuwa wakipinga vita vya Israel huko Gaza Jumatatu walikamatwa wakiwa wameketi nje ya jengo la biashara kuu za hisa mjini New York.
Mgombea urais wa Marekani kwa chama cha Democrat, makamu wa rais Kamala Harris ametangaza mpango wa kuwapa wanaume weusi nafasi zaidi za kiuchumi wakati chama chake kikijaribu kufikia kundi la wapiga kura linaloonekana kutokuwa na ari ya kushiriki kwenye uchaguzi.
Afisa mmoja wa ngazi wa juu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia watoto, UNICEF, amesema Jumatatu kwamba zaidi wa watoto 400,000 wa Lebanon wamekoseshwa makazi ndani ya wiki tatu zilizopita.
Korea Kaskazini Jumapili imesema kuwa wanajeshi wake wa msitari wa mbele wako tayari kufanya mashambulizi dhidi ya Korea Kusini, na kwa hivyo kuongeza hali ya taharuki kwa hasimu wake huyo anayedaiwa kurusha droni zilizoangusha vijikaratasi kwenye mji mkuu wa Pyongyang.
Mwandishi wa habari mwanamke aliyekamatwa na Russia alipokuwa akiripoti mashariki mwa Ukraine amefariki akiwa chini ya ulinzi, maafisa wa Ukraine walitangaza Alhamisi.
Mamlaka nchini Burkina Faso Jumatatu ilifunga matangazo ya VOA kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na maoni yaliyotolewa na mtandao mmoja wa waandishi wa habari.
Wataalam wa haki za binadamu wanaonya kwamba hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imedorora sana kwa mara nyingine huku mapigano kati ya makundi yenye silaha, mashambulizi kwenye shule na hospitali, unyanyasi wa kingono na manyanyaso mengine yakikithiri.
Takwimu za Jumapili kutoka wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza zimeonyesha kuwa wahamiaji 973 waliingia nchini humo kupitia mlango wa bahari unaotokea Ufaransa, huku wengine wanne wakifa wakati wa safari hiyo.
Maafisa wa Palestina wanasema shambulizi la Israel dhidi ya msikiti katika Ukanda wa Gaza limesababisha vifo vya takriban watu 19.
Rwanda ilisema Jumapili imeanza kutoa dozi za chanjo dhidi ya virusi vya Marburg ili kujaribu kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa kama wa Ebola katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, ambapo hadi sasa umeua watu 12.
Raia wa Tunisia walipiga kura siku ya Jumapili katika uchaguzi wa rais, huku mgombea aliye madarakani Kais Saied akitarajiwa kupata miaka mingine mitano madarakani wakati wakosoaji wake wakuu wakiwa gerezani.
Waziri wa Mafuta wa Iran alitua kwenye Kisiwa cha Kharg, katika kituo kikuu cha usafirishaji wa bidhaa hiyo kwenda nje ya nchi, na kufanya mazungumzo na kamanda wa jeshi la majini Jumapili, tovuti ya habari ya wizara ya mafuta Shana iliripoti.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Alhamisi imedhibitishia VOA kuhusu operesheni uliokuwa ngumu ya kuokoa raia wa Iraq na aliyekuwa mtumwa wa ngono kwenye kundi la Islamic State, kutoka Gaza akipitishiwa Israel.
Pandisha zaidi