Maelfu ya waandamanji Alhamisi wamekusanyika kwenye mji mkuu wa Austria, Vienna, kupinga uwezekano wa kurejea madarakani kwa chama cha mrengo wa kulia cha Freedom, FPO, kilicho ongoza kwenye uchaguzi wa kitaifa wa Jumapili.
Uingereza Alhamisi imekubali kuvipatia uhuru wa kujitawala visiwa vya Chagos ambavyo ni zaidi ya 60 vikiwa kwenye Bahari Hindi kwa serikali ya Mauritius, baada ya kuzozaniwa kwa muda mrefu, ikiwa hatua ya kulinda vituo muhimu vya majeshi ya Uingereza na Marekani.
Kuongezeka kwa umaarufu wa vyama vya mrengo wa kulia barani Ulaya kumepelekea wito wa marekebisho makali kwenye sheria ya uhamiaji pamoja na kuzua masuali kuhusu misaada ya kijeshi kwa Ukraine.
Jeshi la Israel limesema Jumatano kwamba wanajeshi wake 8 wameuwawa kwenye mapigano yanayoendelea dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah, kusini mwa Lebanon, siku moja baada ya kuanza kile kilochotajwa kuwa operesheni maalum ya ardhini inayolenga kuharibu miundombinu ya kundi hilo.
Rais wa Marekani Jumatano amemuru kupelekwa kwa wanajeshi 1,000 kwenye shughuli za uokozi katika jamii zilizoathiriwa na kimbunga Helene kusini mashariki mwa Marekani.
Iran Jumanne imefanya shambulizi kubwa la makombora dhidi ya Israel, hatua ambayo inaashiria kusambaa kwa mzozo kati ya Israel na mataifa ya Kiislamu ya kieneo.
Kutokana na janga la kibinadamu linaloendelea kuongezeka Lebanon, Umoja wa Mataifa na serikali ya Lebanon Jumanne wametoa wito wa ufadhili wa dola milioni 426, ili kutoa misaada ya dharura ya moja kwa moja kwa takriban watu milioni moja walioathiriwa na mzozo unaoendelea.
Ripoti iliyotolewa Jumanne imesema kuwa wakati uchaguzi wa Rais wa Marekani ukikaribia, usalama wa wanahabari haujahakikishwa kwa mujibu wa marekebisho ya kwanza ya Katiba ya Marekani.
Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter anatimiza miaka 100 huku waandishi na wanahistoria wakitathmini tena mafanikio yake na kushindwa na pia alikuwa rais wa Marekani wa muhula mmoja tu.
Wakazi wa jimbo la North Carolina Jumatatu walikabiliana na uharibifu mkubwa kutokana na kimbunga Helene, huku mamia ya watu wakiwa hawajulikani walipo, wakati barabara zikiwa zimesombwa na mafuriko pamoja na ukosefu wa huduma muhimu.
Shirika la UN kwa ajili ya wakimbizi wa Palestina, UNRWA, limesema kuwa kamanda wa ngazi ya juu wa Hamas aliyeuwawa nchini Lebanon Jumatatu, alikuwa mmoja wa wafanyakazi wake, lakini hakuwa na jukumu lolote kwa kuwa alisimamishwa kazi kwa muda tangu mwezi Machi.
Idadi ya watu waliokufa nchini Nepal kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyotokana na mvua kubwa mwishoni mwa wiki, imefikia 193, wakati shughuli za uokozi zikiimarishwa Jumatatu.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu limeidhinisha kuongeza muda wa mwaka mmoja zaidi kwa kikosi cha kimataifa cha polisi nchini Haiti kinachosaidiana na polisi wa kitaifa kukabiliana na magenge.
Majimbo ya kusini mashariki mwa Marekani yanaendelea kukabiliana na vifo pamoja na ukosefu wa vifaa muhimu kwenye maeneo ya ndani, huku nyumba zikiharibiwa kutokana na kimbunga Helene, ambacho maafisa wamesema kitakuwa na athari kubwa.
Russia imetangaza Jumapili kwamba waziri wake mkuu Mikhail Mishustin, atakutana na rais wa Iran Masoud Pezeshkian mjini Tehran Jumatatu.
Rais wa Palestina Mahamoud Abbas Alhamisi alitoa wito kwa jumuia ya kimataifa, hasa Marekani, kuacha kuipa silaha Israel ili kukomesha umwagikaji wa damu katika Ukingo wa Magharibi na huko Gaza.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Alhamisi alisema kwamba Israel inapanga kuendelea kushambulia Hezbollah nchini Lebanon “kwa nguvu zote” hadi pale wakazi wa kaskazini mwa Israel watakaporudi majumbani kwao Salama.
Mkuu wa jeshi la Israel Jumatano aliwaambia wanajeshi kujianda kwa ajili ya vita vya ardhini kuivamia Lebanon, huku ndege za kivita za Israel zikishambulia kwa mabomu ngome za Hezbollah kwa siku ya tatu mfululizo.
Israel Jumanne ilishambulia tena ngome za kundi la wanamgambo la Hezbollah nchini Lebanon, huku idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya anga tangu Jumatatu ikiongezeka hadi 564, pamoja na watu 1,835 waliojeruhiwa.
Nigeria imejiunga kwenye orodha kubwa ya viongozi wa Afrika waliopo kwenye mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini New York, kutaka mageuzi kwenye Baraza la Usalama.
Pandisha zaidi