Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 01:53

Takriban watu 200 wafariki kwenye mafuriko ya Nepal


Mto Bagmati unaopitia ndani ya Kathmandu, Nepal, ukiwa umefurika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha. Picha yaJumamosi Sep 28, 2024.
Mto Bagmati unaopitia ndani ya Kathmandu, Nepal, ukiwa umefurika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha. Picha yaJumamosi Sep 28, 2024.

Idadi ya watu waliokufa nchini Nepal kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyotokana na mvua kubwa mwishoni mwa wiki, imefikia 193, wakati shughuli za uokozi zikiimarishwa Jumatatu.

Vifo vingi vimeripotiwa katika mji mkuu Kathmandu ambao ulipata mvua nyingi zaidi na sehemu nyingi za kusini zilikumbwa na mafuriko. Taarifa ya polisi imesema kuwa watu 31 hawajulikani walipo, huku wengine 96 wamejeruhiwa kote kwenye taifa hilo lililopo kwenye milima ya Himalaya.

Maporomoko ya ardhi pia yameripotiwa kuuwa takriban watu darzeni 3 kwenye barabara iliyokuwa haipitiki takriban kilomita 16 kutoka Kathmandu. Maporomoko hayo yalifunika takriban mabasi matatu pamoja na magari mengine ambapo watu walikuwa wamelala kwa kuwa barabara ilikuwa haipitiki.

Barabara kuu tatu za kuingia Kathmandu zilizibwa na maporomoko ya ardhi kwa wikiendi nzima. Hata hivyo kufikia jumatatu, wafanyakazi waliweza kufungua barabara kuu ya Prithvi, kwa kuondoa mawe, matope na miti ambayo ilikuwa imeoshwa na maji kutoka milimani.

Waziri Mkuu wa Nepal Khadga Prasad Oli, amerejea nchini Jumatatu baada ya kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na kuitisha kakao cha dharura, ofisi yake imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG