“Mnaweza kusikia milio ya ndege hapa. Tumeshambulia siku nzima, kwa hiyo nikujianda kwa ajili ya vita vya ardhini na uwezekano wenu wa kuingia lakini pia kuendelea kuishambulia Hezbollah,” Luteni Jenerali Herzi Halevi aliwambia wanajeshi wa kikosi cha vifaru, kulingana na taarifa iliyotolewa na jeshi.
“Hatusitishi. Tunaendelea kushambulia na kuwahujumu kila mahali,” Halevi alisema.
Mkuu huyo wa jeshi alizungumza na wanajeshi saa chache baada ya Hezbollah kurusha kombora la masafa marefu ikilenga makao makuu ya idara ya ujasusi ya Israel (Mossad) karibu na Tel Aviv.
Israel iliangusha kombora hilo, lakini Halevi alionya, akisema “Leo Hezbollah imechochea moto, na baadaye leo, watapata jibu lenye nguvu kubwa. Jiandaeni.”
Israel ilisema pia kwamba imewaanda wanajeshi wa akiba ili kupambana na wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.
Maafisa wa afya wa Lebanon walisema mashambulizi ya Israel yaliua watu wengine 50 Jumatano, na kufanya idadi ya vifo kufikia 615 katika siku tatu, huku wengine zaidi ya 2,000 wakijeruhiwa.
Forum