Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 10, 2024 Local time: 17:54

Vyama vya mrengo wa kulia vyaendelea kushamiri Ulaya


Mwanamke atembea karibu na mabango ya kampeni mjini Vienna, Austria, April 26, 2019. Picha ya maktaba.
Mwanamke atembea karibu na mabango ya kampeni mjini Vienna, Austria, April 26, 2019. Picha ya maktaba.

Kuongezeka kwa umaarufu wa vyama vya mrengo  wa kulia barani Ulaya kumepelekea wito wa marekebisho makali kwenye sheria ya uhamiaji pamoja na kuzua masuali kuhusu misaada ya kijeshi kwa Ukraine.

Chama cha Freedom cha Austria, kilichobuniwa na wa Nazi baada ya Vita Vya Pili vya Dunia, ndicho cha karibuni zaidi cha mrengo wa kulia kupata ushindi mkubwa wa karibu asilimia 29 kwenye uchaguzi wa bunge uliofanyika Jumapili, kikiongoza chama cha People’s kilichopata asilimia 26.

Chama cha Freedom kikiongozwa na Herbert Kicki kilishinda kwa kuahidi kumaliza uhamiaji kwa kuweka ukuta wa Austria, pamoja na kurejeshwa kwa wahamiaji. Chama hicho pia kinapinga misaada ya kijeshi kwa Ukraine pamoja na kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Russia.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Peter Hajek amesema kuwa Kicki aliwavutia wapiga kura kutokana na kuvunjika moyo kwao katika miaka ya karibuni. Vyama vya mrengo wa kulia vinavyopinga uhamiaji vimeshinda uchaguzi wa bunge nchini Uholanzi , Italy na Hungary, uchaguzi wa majimbu wa Ujerumani pamoja na uchaguzi wa bunge la Ulaya nchini Ufaransa mwezi Juni.

Forum

XS
SM
MD
LG