Marekani imepeleka idadi ndogo ya wanajeshi wa ziada huko Mashariki ya Kati kufuatia ongezeko kubwa la ghasia kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon, msemaji wa wizara ya ulinzi Meja Jenerali Pat Ryder alisema Jumatatu.
Israel imezidisha vita vyake dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon Jumatatu, ikiua takriban watu 490 na kujeruhi wengine zaidi ya 1,650 katika mashambulizi makubwa ya anga ambayo yamezua wasiwasi wa kutokea vita vikali.
Mbunge wa siasa za Kimarxist nchini Sri Lanka, Anura Kumar Dissanayake alishinda uchaguzi wa rais kwa ahadi za kuwasaidia watu maskini na kutokomeza ufisadi katika nchi hiyo ambako mdororo wa uchumi miaka miwili iliyopita ulisababisha shinikizo la mabadiliko makubwa.
Mlipuko katika mgodi wa makaa ya mawe mashariki mwa Iran umesababisha vifo vya wafanyikazi 33 na kujeruhi wengine 17, maafisa walisema Jumapili.
Wanamgambo wa Hezbollah wamerusha zaidi ya roketi 100 katika eneo pana la kaskazini mwa Israel, baadhi zikitua karibu na mji Haifa ulio karibu na mpaka kati ya nchi hiyo na Lebanon.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amesikitishwa sana na ripoti za shambulio kubwa dhidi ya jiji la Sudan la al-Fashir na wanamgambo wa RSF na kumtaka kiongozi wake kusitisha shambulio hilo mara moja.
Wanajeshi wa Israel wameshika doria katika eneo linaloshikiliwa na Israel la Golan Heights wakati hali ya wasiwasi inayoendelea kuongezeka mpakani mwa Israel na Lebanon.
Kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, Alhamisi amekiri kwamba shambulizi la wiki hii ndani ya Lebanon kupitia vifaa vya mawasiliano vya kundi hilo, lilikuwa pigo kubwa, huku akisema kuwa Israel ilivuka mipaka hatari kwa kutekeleza operesheni hiyo.
Uamuzi wa Moscow wiki hii wa kupanua uwezo wake wa kijeshi ni dalili ya changamoto inazopitia Russia, kwenye mwaka wa tatu wa uvamizi wake dhidi ya Ukraine, huku ukionekana kujikokota.
White House imetangaza Alhamisi kwamba Rais wa Marekani Joe Biden, Septemba 26 atafanya mazungumzo kwenye Ikulu hiyo na mwenzake wa Ukraine Volodymr Zelenskyy, kuhusu vita vinavyoendelea kati ya taifa lake la Russia.
Wafanyakazi 104 kwenye kiwanda cha elektroniki cha Samsung, waliokuwa wakilalamikia mishahara midogo kusini mwa India Jumatatu wamezuiliwa na polisi kwa tuhuma za kupanga maandamano bila kibali, wakati harakati zao zikisemekana kuathiri shughuli kwenye kiwanda hicho kwa wiki moja iliyopita.
Idadi ya vifo kwenye mataifa ya kati mwa Ulaya imeendelea kuongezeka kufuatia siku kadhaa za mvua kubwa, ambazo zimesababisha mafuriko na kupelelea watu wengi kuondoka makwao.
Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Demokrasia, wachambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania wameeleza kuwa ushiriki mdogo wa wananchi katika masuala ya demokrasia unadhoofisha maendeleo ya kisiasa na kupunguza uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi pamoja na kukwamisha maendeleo ya taifa.
Wahamiaji wanane wameripotiwa kufa Jumapili baada ya boti yao iliojaa kupita kiasi kuzama wakijaribu kuvuka lango la bahari kati ya Ufaransa na Uingereza, kulingana na mamlaka za Ufaransa, ikiwa chini ya wiki mbili tangu kutokea mkasa mbaya zaidi wa aina hiyo mwaka huu.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza David Lammy Jumapili amekosoa rais wa Russia Vladimir Putin kutokana na onyo lake kwamba kuruhusu Ukraine itumie silaha za masafa marefu ndani ya Russia, kutapelekea Moscow kuingia kwenye vita na NATO.
Kombora lililorushwa na waasi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran huko Israel, na kupelekea kulia kwa ving’ora kwenye uwanja wake wa kimataifa wa ndege, ni tukio la karibuni zaidi kwenye majibizano ya kivita tangu kuanza kwa mapigano ya Gaza, wakati Irael ikiashiria kujibu wa njia ya kijeshi.
Mfalme Abdullah wa Jordan amemteua msaidizi wa ngazi ya juu kwenye makao ya kifalme kuwa waziri mkuu baada ya serikali kujiuzulu mapema leo, mahakama ya kifalme imesema.
Rais wa Comoro Azari Assoumani hayupo tena hatarini baada ya kujeruhiwa katika tukio la kuchomwa kisu Ijumaa, na afisa wa polisi mwenye umri wa miaka 24 ambaye alipatikana akiwa amekufa kwenye rumande, maafisa wa usalama wamesema Jumamosi.
Iran Jumamosi imerusha satelaiti kwenye anga za juu kwa kutumia roketi iliyotengenezwa na jeshi, kwa mujibu wa ripoti ya chombo cha habari cha serikali.
Russia na Ukraine Jumamosi zimebadilishana wafungwa, wote wakiwa jumla ya 206, ikiwa ni hatua ya pili kama hiyo, ndani ya siku mbili, kufuatia mashauriano yaliyoongozwa na maafisa wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Pandisha zaidi