Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 14:28

Mashambulizi ya Wahouthi wa Yemen ndani ya Israel yazua wasi wasi


Picha ya maktaba ya waasi wa Houthi wa Yemen
Picha ya maktaba ya waasi wa Houthi wa Yemen

Kombora lililorushwa  na waasi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran huko Israel, na kupelekea kulia kwa ving’ora kwenye uwanja wake wa kimataifa wa ndege, ni tukio la karibuni zaidi kwenye majibizano ya kivita tangu kuanza  kwa mapigano ya Gaza, wakati Irael ikiashiria kujibu wa njia ya kijeshi.

Hakukuwa na ripoti zozote za mauaji au uharibifu, ingawa vyombo vya habari vya Israel vilionyesha watu wakikimbia kuchukua hifadhi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gurion. Mamlaka za uwanja huo zimesema kuwa shughuli za kawaida zilirejeshwa muda mfupi baada ya tukio hilo. Moto ulionekana kwenye eneo la vijijini katikati mwa Israel ambako vyombo vya habari vilionyesha kile kinacho aminika kuwa vifusi kutoka kwa kifaa cha kunasa silaha kilichoanguka kwenye kituo cha treni kwenye mji wa Modiin.

Waasi wa Yemen wanaofahamika kama wa Houthi, wamekuwa wakirusha makombora pamoja na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel tangu kutokea kwa vita vya Israel na kundi la Hamas kwenye Ukanda wa Gaza. Hata hivyo karibu silaha zote zilizorushwa na waasi hao zimenaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel, zikiwa kwenye anga ya bahari ya Shamu. Mwezi Julai, droni inayoaminika kutengenezewa Iran, na iliorushwa na wa Houthi, iligonga mji wa Tel Aviv na kuuwa mtu mmoja, huku ikijeruhi wengine 10.

Forum

XS
SM
MD
LG