Taharuki kati ya Russia na mataifa ya magharibi kuhusu mgogoro huo zimefika viwango vya kutisha wiki hii, kufuatia kikao kati ya rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Uingereza, Kier Starmer, kwenye Ikulu ya Marekani, kuzungumzia iwapo walegeze sheria zinazozuia Kyiv, kutumia silaha za magharibi ndani ya Russia.
Kwa muda sasa, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amekuwa akiomba ruhusa ya kutumia makombora kutoka Uingereza aina ya Storm Shadow, na yale kutoka Marekani ya ATACMS, katika kushambulia malengo ndani ya Russia. Hata hivyo Biden na Starmer walionekana kuchelewesha hatua hiyo baada ya kikao chao cha Ijumaa. Putin kwa muda mrefu ameonya mataifa ya magharibi kuwa yanahatarisha vita vya nyuklia kwa kuunga mkono Ukraine.
Forum