Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kuwa miongoni mwa wa Ukraine 103 waliorejeshwa, 82 walikuwa wanajeshi na wengine 21 ni maafisa. Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kuwa wanajeshi 103 waliorejeshwa walikamatwa kwenye mpaka wa Kursk baada ya vikosi vya Ukraine kufanya shambulizi la kushtukiza la Agosti.
Shirika la habari la UAE la Emirati limesema kuwa UAE iliongoza kwenye upatanishi na kwamba huo ni ubadilishanaji wa 8 tangu vita vilipoanza 2024. Maafisa wa Ukraine katika siku za nyuma walisema kuwa vikosi vya Ukraine vimeshikilia takriban wanajeshi 800 wa Russia, na kwamba hali hiyo ingewasaidia kurejesha wanajeshi wao wanaoshikiliwa na Russia.
Mpatanishi mkuu wa Ukraine, Dmytro Lubinets amesema kuwa baadhi ya wanajeshi wa Ukraine walioachiliwa wamekuwa kizuizini cha Russia tangu mwanzo wa uvamizi huo. Lubinets ameongeza kusema kuwa kufikia sasa wa Ukraine 3,672 wamerejeshwa nchini kufuatia ubadilishanaji wa mara 57.
Forum