Maafisa kaskazini mashariki mwa Ukraine wamesema leo Alhamisi kuwa shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani ya Russia liliwajeruhi watu wasiopungua 14 katika mji wa Konotop.
Shambulio hilo lililenga vituo vya nishati na miundombinu ya raia, maafisa walisema.
Wanajeshi wa Russia pia walielekeza mashambulizi ya drone katika mkoa wa Kherson, ambako maafisa walisema kwamba ulinzi wa anga wa Ukraine ulitungua ndege nne zisizokuwa na rubani.
Jeshi la Ukraine limesema limetungua jumla ya ndege 44 kati ya 64 za Russia zilizotumiwa katika mashambulizi nchini Ukraine.
Mbali na shambulio la Sumy na Kherson, uzuiaji wa shambulio pia ulifanyika kwenye mikoa ya Cherkasy, Dnipropetrovsk, Khmelnytskyi, Kirovohrad, Kyiv, Poltava na Zaporizhzhia.
Forum