Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 22:17

Mafuriko kati kati mwa Ulaya yaendelea kusababisha maafa na uharibifu


Mitaa iliyofurika mjini Opava, katika Jamhuri ya Czech. September 15, 2024.
Mitaa iliyofurika mjini Opava, katika Jamhuri ya Czech. September 15, 2024.

Idadi ya vifo kwenye mataifa ya kati mwa Ulaya imeendelea kuongezeka kufuatia siku kadhaa za mvua kubwa, ambazo zimesababisha mafuriko na kupelelea watu wengi kuondoka makwao.

Baadhi ya mataifa yalioathiriwa ni pamoja na Austria, Jamhuri ya Czech, Poland na Romania, huku Slovakia na Hungary zikitarajiwa kujiunga kwenye orodha hiyo kutokana ma mvua kubwa zinazondelea kunyesha tangu Alhamisi.

Kufikia sasa, watu 6 wamekufa kutokana na mafuriko nchini Romania, mmoja Austria na mwingine Poland. Huko Jamhuri ya Czech, watu wanne hawajulikani walipo baada ya kusombwa na mafuriko, ripoti ya polisi imesema. Sehemu nyingi za Jamhuri ya Czech zimeathiriwa, wakati mamlaka ikitangaza hali ya tahadhari katika zaidi ya sehemu 100 nchini.

Kwenye mji wa Opava, tayari hadi watu 10,000 kati ya jumla ya watu 56,000 wameombwa kuhamia kwenye maeneo salama ya nyanda za juu, Waokoaji walitumia boti kuwasafirisha, kutokana na kufurika kwa mto Opava.

Forum

XS
SM
MD
LG