Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 09, 2026 Local time: 14:47

Raia wa Lebanon wanaoishi Marekani kupewa hifadhi ya muda

Wakazi wa Lebanon wakitoroka mashambulizi ya Israel. Oktoba 15, 2024.(Photo by Maher AL MOUNES / AFP)
Wakazi wa Lebanon wakitoroka mashambulizi ya Israel. Oktoba 15, 2024.(Photo by Maher AL MOUNES / AFP)

Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani Alhamisi imetangaza kanuni mpya zinazotoa ulinzi wa muda kwa baadhi ya wahamiaji wa Lebanon waliopo  Marekani, wakiruhusiwa kuendelea kuishi na kufanya kazi.

Hatua hiyo inajumuisha mpango wa Deferred Enforced Departure DED, pamoja na Temporary Protected Status, TPS, ikiwa imechukuliwa kutokana na kuendelea kwa ghasia nchini mwao. Raia wa Lebanon ambao wameishi mfululizo hapa Marekani tangu Oktoba 16, 2023, wataruhusiwa kuomba hifadhi ya TPS.

Hata hivyo waliowasili baada ya ya tarehe hiyo hawatapewa stakabadhi hizo. Kamati inayopinga ubaguzi dhidi ya Waarabu, ADE imesifu hatua hiyo ya kulinda raia wa Lebanon dhidi ya vita vinavyoendelea, lakini imeomba Marekani kusitisha upelekaji wa silaha kwa Israel, ambazo zinatumika kushambulia Lebanon.

Mkurugenzi mkuu wa kitaifa wa Kamati hiyo Abed Ayoub, amasema kuwa kuhakikisha kuwa raia wa Lebanon waliopo Marekani hawalazimishwi kurudi kwenye hatari ni hatua ya kuridhisha. Hata hivyo amesema kuwa hatua bora zaidi ya kuchuliwa na utawala wa Biden ni kusitisha mara moja upelekaji wa silaha kwa Israel.

This item is part of

Forum

XS
SM
MD
LG