Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 08, 2024 Local time: 17:18

Kamala Harris kuinua hali ya maisha ya wanaume weusi wa Kimarekani


Makamu wa Rais Kamala Harris akiwa kwenye mkutano wa kampeni.
Makamu wa Rais Kamala Harris akiwa kwenye mkutano wa kampeni.

Mgombea urais wa Marekani kwa chama cha Democrat, makamu wa rais Kamala Harris ametangaza mpango wa kuwapa wanaume weusi nafasi zaidi za kiuchumi wakati chama chake kikijaribu kufikia kundi la wapiga kura linaloonekana kutokuwa na ari ya kushiriki kwenye uchaguzi.

Baadhi ya mipango ya Harris ni pamoja na kutoa mikopo inayoweza kusamehewa kwa wawekezaji weusi, kuanzishwa kwa biashara ndogo ndogo, utafiti kwenye ugonjwa wa sickle cell, pamoja na magonjwa mengine ambayo kwa kawaida huathiri wanaume weusi hapa Marekani.

Tayari Harris amesema kuwa anaunga mkono kuhalalishwa kwa bangi pamoja na mpango wake wa kuhakikisha kuwa wanaume weusi wanapata nafasi kwenye sekta ya kitaifa ya uuzaji wa bangi. Pia ameahidi kuratibiwa kwa biashara ya fedha za kidijitali za cryptocurrency, ili kulinda wanaume weusi wanaowekeza kwenye sekta hiyo.

Mpango huo uliopewa jina “opportunity agenda for Black men” unalenga kutoa motisha kwa wanaume wamarekani weusi, ambao wanahofiwa kuwa huenda wakasusia kupiga kura. Mpango huo aliutangaza kabla ya kutembelea mji wa Erie, Penssylvania wenye biashara ndogo za watu weusi, pamoja kufanya mkutano wa kampeni.

Forum

XS
SM
MD
LG