Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 16, 2025 Local time: 23:53

Uchaguzi wa taifa la Georgia wakumbwa na utata


Rais wa Georgia, Salome Zourabichvili akitembelea moja ya vituo vya kupigia kura za bunge mjini Tbilisi, Okt. 26, 2024.
Rais wa Georgia, Salome Zourabichvili akitembelea moja ya vituo vya kupigia kura za bunge mjini Tbilisi, Okt. 26, 2024.

Waendesha mashitaka wa taifa la Georgia wamesema Jumatano kwamba wameanzisha uchunguzi kutokana na uchaguzi wa bunge wa Jumamosi ambao umedaiwa kugubikwa na wizi.

Chama tawala cha Georgia Dream, kilishinda kwa asilimia 54 ya kura zilizopigwa kulingana na tume ya uchaguzi, idadi ambao inakipatia wingi kwenye bunge. Upinzani umedai kuwa uchaguzi huo uliibwa, wakati mataifa ya Magharibi pamoja na waangalizi wa kimataifa wakieleza wasi wasi wao, wakidai kulikuwa na unyanyasaji wa wapiga kura, kununuliwa kwa kura, upigaji kura mara mbili pamoja na ghasia kwenye baadhi ya maeneo.

Upinzani mapema wiki hii uliandamana kwenye barabara za mji wa Tbilisi, wakati ukifanya mkutano wa kukemea matokeo hayo ambayo yametoa muhula mwingine kwa chama tawala. Waendesha mashitaka wamemuita Rais Salome Zourabichvili, ambaye anahusishwa na upinzani unaoungwa mkono na Magharibi kutoa ushahidi wake, lakini amehoji ni kwa nini anahitajika kutoa ushahidi wa wizi wa kura. “Siyo jukumu la Rais la kutoa ushahidi kuhusu wizi wa kura ,”aliambia wanahabari Jumatano.

Forum

XS
SM
MD
LG