Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 16:13

Rais wa Poland asihi Marekani iendelee kusaidia Ulaya


Rais wa Poland, Andrzej Duda akiweka maua kwenye kaburi la kijeshi wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru .Novemba 11, 2024, Warsaw.
Rais wa Poland, Andrzej Duda akiweka maua kwenye kaburi la kijeshi wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru .Novemba 11, 2024, Warsaw.

Rais wa Poland Andzjej Duda Jumatatu ameongoza sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wakati akiomba Marekani iendelee kusaidia Ulaya kwenye masuala ya usalama, ikizingatiwa uvamizi wa Russia wa kieneo, huku akihimiza kuwa mipaka ya Russia ya kabla ya 2014 irejeshwe.

Wengi wanawaza kuhusu vita vinavyoendelea kwa jirani wa Poland, Ukraine na matarajio kwamba kurejea tena kwa Donald Trump kwenye Ikulu ya Marekani kutaleta mabadiliko ya kiusalama kwenye eneo hilo.

Baadhi pia wanaogopa kuwa huenda Trump akaondoa Marekani kwenye NATO, au afanye mkataba na rais wa Russia Vladimir Putin, ambao utahalalisha maeneo ya Ukraine yaliyochukuliwa na Russia, huku Russia ikipata ari ya kivamia mataifa mengine pia.

Baadhi pia wanaamini kuwa Trump ataweza kushawishi Putin kusitisha mapigano hayo. Duda ambaye ana urafiki wa karibu na Trump wakati wa hotuba yake mjini Warsaw amesema kuwa Ulaya itaendelea kuhitaji ulinzi wa Marekani.

Amesema kuwa hakikisho la ulinzi kutoka kwa marais tofauti wa Marekani, ni muhimu sana kwenye nyakati hizi za uchokozi mpya kutoka Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG