Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 09, 2024 Local time: 05:03

Israel na Hezbollah wasitisha mapigano


Gari la askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (UNIFIL) llikiwa kusini mwa Lebanon baada ya shitisho la mapigano kati ya Israel na Hezbollah kuanza kutekelezwa Novemba 27, 2024. Picha na REUTERS/Aziz Taher
Gari la askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (UNIFIL) llikiwa kusini mwa Lebanon baada ya shitisho la mapigano kati ya Israel na Hezbollah kuanza kutekelezwa Novemba 27, 2024. Picha na REUTERS/Aziz Taher

Sitisho la mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah lenye makao yake nchini Lebanon lilianza kutekelezwa mapema Jumatano na hivyo kusimamisha mapigano ambayo viongozi wa Marekani na Ufaransa walisema yanaweza kufungua njia ya kuelekea kwenye sitisho jingine huko ukanda wa Gaza.

Wakati sistisho la mapigano linatekelezwa kulikuwa na msururu wa magari yaliyokuwa yanaelekea kusini mwa Lebanon ambako kwa miezi kadhaa kulikuwa na mapigano makali na kuwalazimisha watu kuhama nyumba zao.

Jeshi la Israel liliwaonya watu kukaa mbali na vijiji vyao ambako iliwahi kuamuru kuondoka.

Wakati huo huo wanajeshi wa ziara wa Lebanon wamepelekwa kusini mwa nchi baada ya kufikiwa sitisho la mapigano kuanza.

Magari ya jeshi la Lebanon yameingia katika Barabara za Tyre na Burj al-Shemali kusini mwa Lebanon, yakipishana na magari ya kiraia yakiwa wamebeba mizigo huku watu wakirejea kwenye nyumba zao baada ya vita kusitishwa wakati jeshi likiongeza idadi ya wanajeshi.

Marekani pamoja na Ufaransa wamekuwa na jukumu kuu katika kusimamia kufikiwa kwa suluhu ambapo baraza la mawaziri la usalama la Israel liliidhinisha jumanne jioni

Rais wa Marekani Joe Biden aliita sitisho la mapigano ni hatua muhimu kumaliza ghasia huko mashariki ya kati. Alisema Iran na washirika wake, hezbolah huko Lebanon na wanamgambo wa Hamas huko Gaza wamelipa gharama kubwa kwa sana kwa zaidi ya mwaka mmoja wa mapiano na wanajeshi wa Israel.

Baadhi ya taarifa ya habari hii inatoka Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG