Vikosi vya Israel siku ya Ijumaa vilishambulia maeneo ya Ukanda wa Gaza, huku mashahidi wakiripoti uvamizi wa angani kuzunguka mji wa kusini wa Rafah, eneo ambalo limekuwa likiangaziwa zaidi katika vita vya karibu miezi minane.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun, walifanya mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana pembezoni mwa mazungumzo ya Shangri-La nchini Singapore siku ya Ijumaa.
Rais wa China Xi Jinping Alhamisi ameomba kuwepo kwa kongamano la amani la kumaliza vita kati ya Israel na Hamas, wakati alipokuwa akihutubia viongozi wa kiarabu kwenye kikao kinacholenga kuimarisha uhusiano na mataifa yao.
Matokeo ya awali katika uchaguzi wa Afrika Kusini yanakiweka chama cha tawala , ANC kwenye kiwango cha zaidi ya 42% ya kura, kikiongeza uwezekano kwamba huenda kikapoteza wingi wake kwa mara ya kwanza tangu kilipokamata madaraka 1994.
Majadiliano ya jopo la mahakama yalianza Jumatano katika kesi ya Donald Trump ya malipo ya kumnyamazisha mwanamke mcheza filamu za ngono, hivyo kuweka matokeo ya kesi hii ya kihistoria mikononi mwa wakazi kumi na wawili wa New York.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kukutana Jumanne kujadili hali ya Rafah kufuatia shambulizi la anga la Israel lililoua Wapalestina 45 waliokuwa wakijihifadhi katika kambi ya wakimbizi na kuwajeruhi wengine 200.
Jeshi la Israel linatathmini tukio katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza baada ya maafisa wa afya kusema kulikuwa na mashambulizi ya Israel ambayo yameua raia 35 jana Jumapili.
Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa imeiamuru Israel siku ya Ijumaa kusitisha mara moja operesheni zake za kijeshi katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza - lakini iliacha kuamuru sitisho kamili la mapigano.
Marekani itaitambua Kenya kama mshirika wake wa kwanza asiyekuwa mwanachama wa NATO katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara, White House imesema wakati Rais Joe Biden alipomkaribisha Rais William Ruto katika ziara ya kiserikali.
Mwendesha mashtaka mkuu kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Jumatatu amesema anataka kuomba hati ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi Yoav Gallant, pamoja na kiongozi wa Hamas huko Gaza Yahya Sinwar kuhusiana na vita vya Israel na Hamas.
Pakistan imetangaza siku moja ya maombolezo, nayo Lebanon imetangaza siku tatu za maombolezo, huku serikali kadhaa zikitoa salamu za rambirambi kwa Iran baada ya kifo cha Rais Ebrahim Raisi na waziri wa mambo ya nje Hossein Amirabdollahian katika ajali ya helikopta.
Hospitali moja ya Gaza ilisema Jumapili kwamba shambulio la anga la Israel lililolenga nyumba moja katika kambi ya wakimbizi katikati mwa ardhi ya Palestina liliua takriban watu 20.
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel wa Iran aliyefungwa gerezani, Narges Mohammadi, anakabiliwa na kesi mpya kuhusu tuhuma alizotoa dhidi ya vikosi vya usalama kuwanyanyasa kingono wafungwa wa kike, familia yake ilisema Jumamosi.
Mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua kubwa za msimu magharibi mwa Afghanistan yamesababisha vifo vya takriban watu 50 na wengine kadhaa hawajulikani walipo, afisa wa Taliban alisema Jumamosi, akiongeza kuwa idadi ya waliofariki ilitokana na ripoti za awali na huenda ikaongezeka.
Rais Xi Jinping wa China alisifu uhusiano kati ya China na Russia Alhamisi, na kuahidi kuuimarisha, alipokuwa akimkaribisha Rais wa Russia Vladimir Putin kwa mazungumzo mjini Beijing.
Idadi kubwa ya wapiga kura vijana katika uchaguzi wa rais Marekani wanasema wanatamani wangekuwa na mtu mwingine na siyo Joe Biden au Donald Trump kumchagua.
Huku Marekani hivi karibuni iliamua kusitisha usafirishaji wa baadhi ya shehena kwa Israel, vita huko Gaza sasa vimekuwa ni sehemu ya mjadala mkali sana kuhusu kampeni ya Rais wa Marekani.
Kiongozi wa upinzani nchini Chad Succes Masra amewasilisha rufaa ya kisheria kwa baraza la katiba la nchi hiyo kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais, uliofanyika tarehe 6 mwezi huu, nchini humo.
Umoja wa Mataifa na mamlaka za Taliban Jumamosi wamesema idadi ya vifo kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa za msimu zilizonyesha katika jimbo la kaskazini mwa Afghanistan la Baghlan imeongezeka na kufikia watu 300.
Kundi la wanamgambo wa Hamas limetoa taarifa Jumatatu likiridhia pendekezo la sitisho la mapigano la Misri na Qatar. Wapatanishi mjini Cairo wamekuwa wakijaribu kusimamisha mapigano kwa muda na kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa na Hamas huko Gaza.
Pandisha zaidi