Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 00:16

Hamas yakubali pendekezo la sitisho la mapigano la Misri na Qatar

Khalil al-Hayya, Afisa mkuu aliyewakilisha Hamas katika mazungumzo ya kutisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka, akizungumza katika mahojiano na Associated Press, mjini Istanbul, Aprili 24, 2024.
Khalil al-Hayya, Afisa mkuu aliyewakilisha Hamas katika mazungumzo ya kutisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka, akizungumza katika mahojiano na Associated Press, mjini Istanbul, Aprili 24, 2024.

Israel ilikuwa haijatoa msimamo wake, ambapo jeshi lake Jumatatu lilisema watu katika maeneo ya mashariki mwa mji wa Rafah wanapaswa kuelekea kwenye eneo ambalo jeshi limeliita eneo kubwa la kibinadamu ambalo linajumuisha Khan Younis, katika hatua ambayo inajiri kabla ya shambulizi lililopangwa la Israel huko Rafah.

Msemaji wa jeshi la IDF akiandika kwenye mtandao wa kijamii kwa Kiarabu, amesema jeshi la Israel litachukua hatua kali dhidi ya taasisi za kigaidi huko Rafah, na kwamba yeyote ambaye yuko katika eneo hilo atakuwa ameyaweka maisha yake hatarini.

Israel inaandaa “operesheni ya wigo mdogo” huko Rafah, msemaji wa jeshi amesema, na inakadiriwa watu 100,000 ndio wameombwa kuondoka katika eneo la uokoaji.

Forum

XS
SM
MD
LG