Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:39

Mshindi wa Tuzo ya Nobel aliye gerezani Iran akabiliwa na kesi mpya


Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel wa Iran aliyefungwa gerezani, Narges Mohammadi.
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel wa Iran aliyefungwa gerezani, Narges Mohammadi.

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel wa Iran aliyefungwa gerezani, Narges Mohammadi, anakabiliwa na kesi mpya kuhusu tuhuma alizotoa dhidi ya vikosi vya usalama kuwanyanyasa kingono wafungwa wa kike, familia yake ilisema Jumamosi.

Kesi hiyo, inayotarajiwa kuanza Jumapili, inahusiana na ujumbe wa sauti alioutoa akiwa gerezani mwezi Aprili ambao pia ulisambazwa na wafuasi wake ambapo alishutumu kile alichokiita "vita kamili dhidi ya wanawake" katika Jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Anashtakiwa katika kesi hii ya hivi punde kwa kueneza "propaganda dhidi ya serikali," familia yake ilisema.

Hakujawa na maoni yoyote juu ya kesi hiyo kutoka kwa mamlaka ya mahakama ya Iran.

Familia yake ilimnukuu Mohammadi akisema kesi hiyo inapaswa kufanywa hadharani ili "mashahidi na walionusurika watoe ushahidi wa unyanyasaji wa kingono unaofanywa na utawala wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya wanawake."

Mohammadi, ambaye amefungwa katika jela ya Evin ya Tehran, aliwataka wanawake wa Iran katika ujumbe wake wa Aprili kupitia ukurasa wake wa Instagram kuelezea wazi kuhusu kukamatwa kwao, na unyanyasaji wa kijinsia mikononi mwa mamlaka.

Forum

XS
SM
MD
LG