Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:00

Chad: Kiongozi wa upinzani awasilisha rufaa kupinga matokeo ya uchaguzi


Chad Election
Chad Election

Kiongozi wa upinzani nchini Chad Succes Masra amewasilisha rufaa ya kisheria kwa baraza la katiba la nchi hiyo kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais, uliofanyika tarehe 6 mwezi huu, nchini humo.

Baraza la kitaifa la usimamizi wa uchaguzi, linalosimamiwa na serikali, siku ya Alhamisi lilimtangaza Rais wa mpito Mahamat Idriss Deby mshindi wa uchaguzi huo, kwa asilimia 61.3 ya kura, kwa mujibu wa matokeo ya awali, huku Masra ikishika nafasi ya pili kwa asili mia 18.53.

Hata hivyo, kabla ya tangazo hilo rasmi, Masra, ambaye anahudumu kama waziri mkuu wa serikali ya mpito, alisema alishinda ushindi, na kudai kuwa kulikuwa na mipango ya udanganyifu katika uchaguzi.

"Kwa msaada wa mawakili wetu,...tuliwasilisha ombi kwa Baraza la Katiba kufichua ukweli wa masanduku ya kura," Masra alisema katika mjumbe kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na X Jumapili, akiwataka wafuasi wake kuwa watulivu.

Forum

XS
SM
MD
LG