Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Afrika, ANOCA, Mustapha Berraf, amesema Jumapili kwamba Misri itawasilisha ombi la kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya 2036, pamoja na ile ya msimu wa joto ya 2040.
Mahakama ya kijeshi ya Sierra Leone imetoa hukumu ya vifungo virefu vya jela kwa wanajeshi 24 kutokana na jaribio la kupindua serikali ya Rais Julius Maada Bio, Novemba mwaka uliopita.
Rais wa Kenya William Ruto ameongoza hafla ya kuapishwa kwa baraza jipya la mawaziri, jijini Nairobi, wakiwemo mawaziri wanne wa upinzani akiwapa jina la “timu ya mahasimu,” baada ya majuma kadhaa ya maandamano ambayo kuna wakati yalikuwa ya ghasia.
Msemaji wa idara ya usalama ya jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kano, Peter Afunanya, amesema Jumatano kuwa Nigeria wiki hii imewakamata raia 7 wa Poland, kwa kupeperusha vibendera vya Russia wakati wa maandamano dhidi ya serikali.
Marekani imesema Jumatano kwamba itatoa karibu dola milioni 414 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa Jamhuri ya Kidemokarasi ya Congo, ambako zaidi ya watu milioni 25 wanahitaji misaada hiyo, ikiwa ni takriban robo ya wakazi nchini humo.
Serikali ya Uturuki itafanya mazungumzo na maafisa wa Instagram Jumatatu baada ya mtandao huo wa kijamii kufunga fursa ya kuingia kwenye jukwaa la hilo wiki iliyopita, Waziri wa Usafiri na Miundombinu Abdulkadir Uraloglu alisema katika ujumbe kwenye mtandao wa X.
Polisi nchini Nigeria wamekuwa katika hali ya tahadhari leo Ijumaa, na huenda wakaomba msaada wa wanajeshi, baada ya maandamano kuzua vurugu katika baadhi ya miji.
Marekani imeendeleza kasi yake ya ushindi kwa medali ya tano mfululizo ya dhahabu ya Olimpiki kwa ushindi wa pointi 103-86 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo wa mpira wa kikapu wa wanaume,
Picha za video zilizochukuliwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani imeonyesha wanajeshi pamoja na timu za uokozi wakipekuwa kwenye matope na mawe katika eneo la Kerala, India.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema leo kusiwepo na kitu chochote ambacho kitaondoa umuhimu wa kufikia sitisho la mapigano huko Gaza, baada ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh kuuwawa mapema nchini Iran.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan Jumapili alisema kwamba Uturuki inaweza kuingia Israel kama ilivyofanya katika miaka iliyopita huko Libya na Nagorno-Karabakh, licha ya kuwa hakufafanua zaidi kuhusu uingiliaji kati huo.
Mkuu wa sheria wa Libya amesema Jumapili kwamba mahakama imewafunga gerezani maafisa 12, kutokana na kuporomoka kwa mabwawa kadhaa mjini Derna, mwaka uliopita, ambapo maelfu ya wakazi walikufa.
Kundi moja la wanaharakati wa demokraisa nchini Sudan limesema Jumamosi kwamba tariban watu 22 wameuwawa baada ya kundi la kijeshi lenye silaha la Rapid Support Forces, RSF, kushambulia mji wa al-Fashir.
Rais wa Kenya William Ruto, Alhamisi amemteua Douglas Kanja, kuwa Inspekta Jenerali wa polisi, ofisi yake imesema, ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na mkuu wa zamani Japhet Koome, aliyejiuzulu kufuatia shutuma kwa namna alivyoshughulikia maandamano dhidi ya serikali.
Siku kadhaa baada ya kukatishwa safari za ndege, abiria waliendelea kusubiri huku wakiwa wamekata tamaa Jumatatu katika uwanjwa wa ndege wa Hartsfield-Jackson, Atlanta.
Kamanda wa jeshi katika kikosi maalum cha Hezbollah cha Radwan aliuawa katika shambulio la Israel kusini mwa Lebanon, jeshi la Israel na vyanzo viwili vya usalama vilisema Alhamisi.
Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan amethibitisha katika mazungumzo na mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan, kwamba nchi yake inaunga mkono juhudi zinazolenga kumaliza mzozo nchini Sudan, shirika la habari la serikali ya Emirati WAM liliripoti Alhamisi.
Polisi nchini Kenya walifyatua gesi ya kutoa machozi Jumanne kuwatawanya mamia ya waandamanaji wenye lengo la kuweka shinikizo zaidi kwa Rais William Ruto, hata baada ya kuafiki matakwa ya waandamanaji katika siku za nyuma.
Umoja wa Ulaya Jumatatu ulitangaza vikwazo dhidi ya Waisraeli watano na mashirika matatu, ukiwaelezea kuwa ni wahusika wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu” dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki.
Pandisha zaidi