Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 08, 2024 Local time: 18:58

Misri kuwasilisha ombi la kuwa mwenyeji wa Olimpiki ya 2036


Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki,Thomas Bach.
Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki,Thomas Bach.

Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Afrika, ANOCA, Mustapha Berraf, amesema  Jumapili kwamba Misri itawasilisha ombi la kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya 2036, pamoja na ile ya msimu wa joto ya 2040.

Hilo linafanyika wakati ikiendelea kuimarisha miundomsingi yake pamoja na viwanja vya michezo, ili kufanikisha ombi hilo. Mustapha Berraf ameyasema hao wakati wa kufungwa rasmi kwa michezo ya Olimpiki ya 2024, mjini Paris, Ufaransa.

Afrika haijawahi kuwa mwenyeji wa Olimpiki, na Cairo mara ya mwisho ilifanya ombio hilo kwenye Olimpiki za 2008. Likiwa taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu kwenye Ukanda wa kiarabu, Misri imetumia mabilioni ya fedha kujenga viwanja vya michezo katika miaka ya karibuni kama sehemu ya mpango wa kulifanya taifa la kisasa.

Mji mpya wa Olimpiki mashariki mwa Cairo ulianza kutumika kama makao makuu ya kiutawala 2015, ukitarajiwa kuwa na kiwanja cha michezo chenye uwezo wa kupokea watu 93,000, pamoja na kuwepo kwa viwanja vingine 21. Berraf mwenye asili ya Algeria amesema kuwa taifa lingine lenye uwezo wa kuomba kuwa mwenyeji wa michezo hiyo ni Afrika Kusini.

Forum

XS
SM
MD
LG