Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 21:38

Umoja wa Falme za Kiarabu unaunga mkono juhudi za kumaliza mzozo wa Sudan


Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mohammed bin Zayed al-Nahayan
Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mohammed bin Zayed al-Nahayan

Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan amethibitisha katika mazungumzo na mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan, kwamba nchi yake inaunga mkono juhudi zinazolenga kumaliza mzozo nchini Sudan, shirika la habari la serikali ya Emirati WAM liliripoti Alhamisi.

Wakati wa mazungumzo hayo kwa njia ya simu, Sheikh Mohammed “alithibitisha niya ya Umoja wa Falme za Kiarabu kuunga mkono suluhuhisho na juhudi zote zinazolenga kukomesha ghasia na kumaliza mzozo nchini Sudan kwa njia ambayo inachangia kuimarisha utulivu na usalama wa Sudan na kutimiza matarajio ya wanachi wake,” WAM iliongeza.

Yalikuwa mazungumzo ya kwanza ya hadharani kati ya viongozi hao wawili tangu uhusiano wao ulipodorora mwaka jana.

Jeshi la Sudan lilishutumu Umoja wa Falme za Kiarabu katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Juni kuunga mkono hasimu wake, kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces( RSF), katika mzozo wa nchi hiyo uliodumu miezi 15, shutuma ambazo taifa hilo la Ghuba lilizikanusha.

Mwezi Aprili mwaka jana, vita vilizuka kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa Rapid Support Forces juu ya uongozi wa mpito na uchaguzi huru.

Umoja wa Mataifa unasema kutokana na vita karibu watu milioni 25, nusu ya wananchi wa Sudan, wanahitaji msaada, kuna hatari ya njaa na watu milioni 10 walikimbia makazi yao.

Forum

XS
SM
MD
LG