Habib Maatuk alichukua nafasi ya kamanda mwingine katika kikosi hicho maalum, Ali Ahmed Hussein ambaye aliuawa mwezi Aprili katika shambulio la Israel, vyanzo vya usalama vilisema.
Jeshi la Israel lilisema lilimua kamanda wa operesheni za kikosi cha Radwan likimtambulisha kama Jaafar Maatuk, pamoja na kamada mwingine anayehusika na operesheni za kikosi cha Radwan katika jimbo la Hajir.
Limesema wapiganaji zaidi wa kikosi cha Radwan waliuawa katika shambulio hilo.
Kiongozi wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah alionya katika hotuba siku ya Jumatano kwamba kundi lake litapanua wigo wa mashambulizi yake nchini Israel ikiwa Israel itashambulia raia zaidi.
Mapema Alhamisi, Hamas ilisema mmoja wa makamanda wake aliuawa katika shambulio la Israel eneo la Bekaa magharibi mwa Lebanon na kamanda wa Hezbollah aliuawa katika shambulio la Israel katika mji wa kusini wa Jbal el Botm.
Forum