Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:39

Rais Ruto aapisha baraza jipya la mawaziri wakiwemo wa upinzani


Rais William Ruto akipeana mkono na waziri mpya kutoka upinzani Hasan Ali Joho wakati wa kuapishwa kwa baraza lake jimpya la mawaziri huko Nairobi Agosti 8, 2024 Picha na Reuters
Rais William Ruto akipeana mkono na waziri mpya kutoka upinzani Hasan Ali Joho wakati wa kuapishwa kwa baraza lake jimpya la mawaziri huko Nairobi Agosti 8, 2024 Picha na Reuters

Rais wa Kenya William Ruto ameongoza hafla ya kuapishwa kwa baraza jipya la mawaziri, jijini Nairobi, wakiwemo mawaziri wanne wa upinzani akiwapa jina la “timu ya mahasimu,” baada ya majuma kadhaa ya maandamano ambayo kuna wakati yalikuwa ya ghasia.

Rais Ruto aliyefanya kampeni kwa ajili uchaguzi wa Agosti 2022, alijiita kama mtu wa watu, lakini maandamano ya ghasia yanayopinga sera zake za uchumi yameharibu sura yake ndani ya nchi na kuchafua msimamo wake nje ya nchi, wamesema wachambuzi.

Kiongozi huyo anayekabiliwa na ukosoaji mkubwa tangu aliposhinda uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali, huku kukiwa na hali kutoridhishwa – vijana wanaojiita Gen Z waliongoza maandamnano – katika taifa ambalo kwa kawaida linaelezewa lina utulivu na mataifa ya Magharibi katika eneo ambalo mara nyingi lina vurugu.

James Opiyo Wandayi wakati aliapishwa
James Opiyo Wandayi wakati aliapishwa

Maandamano hao yamechochewa na pendekezo la ongezeko la kodi katika mswada wa fedha wa mwaka 2024, na kuleta hali ya wasi wasi mkubwa kuhusu mtindo wa uongozi wa Rais Ruto wa kuanzia juu kwenda chini, na kusababisha mzozo mkubwa kwa urais wake –na utawala wake ukijikuta umeshtukizwa na kinachotokea.

Takribani watu 60 wameuawa tangu maandamano kuanza katikati ya mwezi Juni, wakati polisi walipotumia risasi za moto kwa waandamanaji, darzen za watu wamepotea, kulingana na umoja wa makundi ya ushawishi yakiwemo tume ya haki inayofadhiliwa na serikali KNCHR na Amnesty Kenya.

Muandamanaji akiwa amewekwa kizuizini na maafisa wa usalama huko Nairobi Agosti 8, 2024
Muandamanaji akiwa amewekwa kizuizini na maafisa wa usalama huko Nairobi Agosti 8, 2024

Awali Ruto aliuelezea msukosuko huo unahusu kile Wakenya wanachokiona kuwa kuenea kwa ufisadi serikalini na ukosefu wa ufanisi kuwa “uhaini” na kuapa kumaliza machafuko “katika gharama yoyote.

Lakini baadaye alirudi nyuma, akizungumzia mfululizo wa hatua kali za kushughulikia hasira za wananchi ikiwa pamoja na kuuondoa mswada wa fedha , kulivunja baraza lake la mawaziri na kupunguza bajeti kwa kiwango kikubwa.

Forum

XS
SM
MD
LG