Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 22:43

Abiria wakwama uwanja wa ndege kufuatia hitilafu ya mtandao


Abiria wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hartsfield-Jackson, Atlanta, Juni 21, 2024. Picha na Charly TRIBALLEAU / AFP.
Abiria wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hartsfield-Jackson, Atlanta, Juni 21, 2024. Picha na Charly TRIBALLEAU / AFP.

Siku kadhaa baada ya kukatishwa safari za ndege, abiria waliendelea kusubiri huku wakiwa wamekata tamaa Jumatatu katika uwanjwa wa ndege wa Hartsfield-Jackson, Atlanta.

Shirika la ndege la Delta linaendelea kuhangaika kurejesha safari zake, siku ya tatu baada ya hitilafu ya mtandao duniani iliyo sumbua safari za ndege sehemu mbalimbali duniani na kusababisha maelfu ya wasafiri kukwama.

Shirika hilo la ndege lenye ofisi zake Atlanta limekatisha safari za ndege 778, au takribani asilimia 20, mpaka kufikia saa saba na nusu mchana wa Jumatatu, kwa mujibu wa FlightAware. Inaakuwa nusu ya jumla ya safari zilizo katishwa.

Waziri wa usafiri wa Marekani, Pete Buttigieg alisema Jumapili, ofisi yake imepokea mamia ya malalamiko kuhusiana na kitengo cha huduma za wateja cha Delta na watu wakitaka kurudishiwa pesa zao haraka.

Forum

XS
SM
MD
LG