Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 03:17

WHO yaeleza kilichosaidia kudhibiti haraka Ebola DRC


Wakazi wa Congo waungana na wafanyakazi wa Shirika la Madaktari bila ya Mipaka (MSF) wakijiandaa na chanjo ya pili ya Ebola katika eneo la Majengo mjini Goma.
Wakazi wa Congo waungana na wafanyakazi wa Shirika la Madaktari bila ya Mipaka (MSF) wakijiandaa na chanjo ya pili ya Ebola katika eneo la Majengo mjini Goma.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema waliojifunza kutokana na milipuko ya awali ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ni tiba muwafaka ziliruhusu kupata udhibiti wa haraka wa ugonjwa huu ambao unasababisha vifo katika jimbo la Equateur.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanaripoti hakuna uhusiano kati ya mlipuko wa Ebola uliotangazwa Juni 1 huko Mbandaka, jimbo la Equateur, na mlipuko, ambao ulizuka karibu miaka miwili iliyopita nchini DRC katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Meneja operesheni za dharura katika WHO, Michel Yao anasema shirika la Afya Duniani lina zaidi ya wafanyakazi 20 huko na liko tayari kupeleka watu zaidi, kama ni muhimu. Ameiambia VOA kwamba WHO inafanya kazi na washirika wake kufungua vituo vya matibabu, kuafuatilia hatari zitakazojitokeza na kujibu kwa haraka na kuzitambua kesi mpya.

“Lengo letu kwa wakati huu ni kufanya kazi na maafisa wa kieneo ambao tayari wamepatiwa. Walikuwa na ujuzi fulani. Kwa hiyo, inabidi tubuni mkakati mpya na kubaki kuwapatia mafunzo na maelekezo. Somo tulilojifunza ambalo limebaki ni kufanya kazi na jamii,” Yao amesema.

Mlipuko wa mashariki mwa DRC, ambao uliwaathiri zaidi ya watu 3,460 na kuua watu 2,280 hatimaye ulionekana kuanza kupungua kabisa. Ripoti za karibuni kutoka magharibi mwa DRC, ambako mlipuko ndiyo kuanza umejitokeza, na kuweka idadi ya kesi ambazo zimethibitishwa ni 12 ikiwemo vifo tisa.

Miaka miwili iliyopita, eneo hilo hilo lilikumbwa na Ebola. Ilichukua takriban kipindi cha chini ya miezi minne kudhibiti mlipuko kwamba msaada wa chanjo ya majaribio, ambayo ilitolewa kuwalinda watu dhidi ya virusi.

Yao anasema chanjo, ambayo tangu ithibitishwe kuwa ni salama na ifanya kazi, itasaidia kuharakisha kudhibiti virusi. Hadi hivi sasa, zaidi ya watu 600 wamepatiwa chanjo katika Mbandaka na Wangata. Anasema dozi 3,000 za chanjo zimepatika na zinatarajiwa kupelekwa hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG