Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 10:37

Huenda mlipuko mpya wa Ebola ukaenea tena DRC - WHO


Picha ya virusi vya Ebola

Mlipuko wa ugonjwa wa  Ebola mashariki mwa Kongo unaweza kuenea tena baada ya mgonjwa mmoja kutoroka kutoka kwenye kliniki, na kupelekea ugumu katika udhibiti wa ugonjwa huo ambao umeambukiza watu sita tangu wiki iliyopita, shirika la Afya ya Ulimwenguni -WHO lilieza  Jumapili.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa imebakiza siku mbili tu kabla ya kutangaza kumalizika kwa janga la pili la ugonjwa mkubwa wa Ebola wakati mlolongo mpya wa maambukizo uliogunduliwa mnamo Aprili 10, kufuatia zaidi ya wiki saba bila kesi mpya. Tangu wakati huo, viongozi wa afya wametafuta njia za kuzuia maambukizo yoyote mapya. Lakini Ijumaa dereva wa boda boda mwenye umri wa miaka 28 ambaye alikuwa amepimwa virusi vya Ebola alikimbia kutoka kituo ambacho alikuwa akitibiwa katika mji wa Beni. Chanjo mbili mpya zimekuwa na athari kubwa katika kuzuia Ebola, lakini mashambulizi ya wanamgambo yamezuia wafanyakazi wa afya kufikia maeneo kadhaa yaliyoathiriwa na virusi hivyo nchini DRC.

-Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG