Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 22:05

White House ina mashaka iwapo mazungumzo ya Putin na Xi yatapelekea kumalizika vita Ukraine


Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa China Xi Jinping wakisherehekea mkutano wao nchini Moscow, Russia.

Wakati Xi Jinping akikamilisha ziara yake ya siku tatu huko Moscow, White House imeelezea mashaka yake kwamba mazungumzo ya kiongozi wa China na Rais wa Russia Vladimir Putin yamefungua njia ya kumaliza vita nchini Ukraine.

Mjini Moscow, alipewa heshima ya zulia jekundu na chakula cha jioni ambapo aliandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Russia Vladimir Putin kwa ajili ya kiongozi wa China Xi Jinping.

“Kama wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, China na Russia itaendelea kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa kulinda kanuni za msingi za uhusiano wa kiamtaifa kulingana na malengo na misingi ya mkataba wa Umoja wa Mataifa,” anasema Rais Xi.

Xi alitaka lipatikane suluhisho la kidiplomasia nchini Ukraine ambapo Putin anasema anaunga mkono. “Tunaamini kwamba mambo mengi katika mpango wa amani wa China yanafanana na mwelekeo wa Russia na huenda ikawa msingi suluhisho la amani, wakati Magharibi na Kyiv watakapokuwa tayari kwa hilo. Hata hivyo, hatuoni aina yoyote ya utayari kwa upande wao mpaka hivi sasa.”

White House imelipinga dai la Putin. John Kirby wa Baraza la Usalama anasema “hatujaona kitu chochote walichosema, ambacho wamekiweka mbele, hiyo inatupa matumaini kwamba vita hivi huenda vikamalizika wakati wowote ujao.”

Kabla ya mkutano wa Putin na Xi, Marekani ilionya dhidi ya makubaliano ya sitisho la mapigano linalosimamiwa na wachina, ikisema kuwa huenda wakaidhinisha mafanikio ya Russia nchini Ukraine.

Mkutano wa Putin na Xi hawakutoa pendekezo lolote kwa mashauriano ya sitisho la mapigano, John Kirby alisema kuwa Marekani itaiunga mkono Beijing kama itasimamia mazungumzo hayo kama Rais Volodymyr Zelenskyy ataamaini kuwa huenda yatapelekea upatikanaji wa amani. Kwa kiongozi wa Ukraine, hiyo ina maana kufikia maridhiano kwa maeneo ambayo Putin amejiingiza kwa nguvu.

George Beebe, mkurugenzi wa Grand Strategy katika taasisi ya Quincy for Responsible Statecraft akizungumza kwa njia ya Skype alielezea mtizamo wake. “Nina mashaka kwamba warussia watakubaliana na sharti hilo. Tayari wamelikataa kama kitu ambacho wanahisi haihusiani na masuala ya mashauriano.”

Zelenskyy alikutana Jumanne na Fumio Kishida. Waziri Mkuu wa Japan akiwa kiongozi wa karibuni mshirika wa Magharibi aliyefanya ziara ya kushtukiza huko Kyiv.

“Kutokana na nguvu ya Japan, uongozi wake huko Asia ni kutetea amani na kanuni za utaratibu wa kimataifa, na jukumu la Japan kama mwenyekiti wa G-7, mazungumzo yetu leo kwa kweli yanaweza kuwa na matokeo duniani,” amesema Zelenskyy

Baada ya mkutano na Putin, mazungumzo ya simu kati ya Xi na Zelenskyy huenda pia yakafanyika, lakini hilo bado halijathibitishwa.

XS
SM
MD
LG