Hatua hiyo ni baada ya Putin kukaribisha mpango wa amani wa Beijing wa kutatua vita vya Russia dhidi ya Ukraine na kuwaashiria viongozi wa nchi za Magharibi kiwango cha kile wanachoita urafiki wao usio na kikomo.
Xi alisema Jumanne alimwalika Putin kuitembelea China baadaye mwaka huu.
Katika matamshi yake ya ufunguzi kabla ya mazungumzo yao ya faragha Jumatatu, Putin alisema Russia inafurahishwa na maendeleo ya haraka ya China katika miongo ya karibuni ambayo yameikuza na kuwa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani nyuma ya Marekani.
Mashirika ya habari ya Russia baadaye yaliripoti viongozi hao walizungumza kwa takriban saa nne na nusu kabla ya chakula cha jioni, ambapo msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema Putin angempa Xi maelezo ya kina kuhusu hatua za Moscow nchini Ukraine.