Wakati ikitangaza sheria mpya na viwango vya utendakazi, mkurugenzi mkuu wake Shou Zi Chew ameonya dhidi ya uwezekano wa Marekani kupiga marufuku App hiyo maarufu ya China. Chew amepangwa kuzungumza mbele ya wabunge wa Marekani Alhamisi, wakati wakimhoji kuhusu sera za usalama wa taarifa kupitia TikTok, pamoja na uhusiano wake na serikali ya China.
Chew kupitia video ya TikTok amesema kwamba mahojiano hayo yamekuja wakati muhimu kwa kampuni yake,baada ya wabunge wa Marekani kubuni hatua zitakazowezesha utawala wa Biden kupiga marufuku App hiyo hapa Marekani ambako ina zaidi ya watumizi milioni 150.
Chew wakati akizungumza mbele ya wanahabari karibu na majengo ya bunge la Marekani alisema kwamba pendekezo la baadhi ya wabunge wa Marekani la kupiga marufuku TikTok litaathiri wamarekani milioni 150.