Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 07:18

Watu 20 wafariki Kenya baada ya basi kutumbukia mtoni


Ramani ya Kenya na nchi jirani
Ramani ya Kenya na nchi jirani

Watu wasiopungua 20 wa kwaya ya Kanisa Katoliki la Mwingi wamefariki baada ya basi walilokuwa wanasafiria kutumbukia katika Mto Enziu, kaunti ya Kitui, kusini mashariki mwa Kenya, Jumamosi.

Hadi sasa, miili 20 imepatikana kutoka katika basi na watu wengine 10 wameokolewa na kupelekwa katika Hospitali ya Mwingi Level Four kwa matibabu ya dharura.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kitui Leah Kithei, basi hilo yenye siti 51 linalomilikiwa na Mwingi Junior Seminari, Shule binafsi inayoendeshwa na Kanisa Katoliki, ilikuwa inawasafirisha wana kwaya kwenda eneo la Nuu kutoka mji wa Mwingi kuhudhuria sherehe za harusi.

Bi Kithei amesema polisi walifika katika eneo la ajali kuratibu juhudi za uokoaji zilizokuwa zimedumazwa na mfumuko wa maji.

“Tunatarajia kuwaokoa watu wengi kadiri ya uwezo wetu. Cha kusikitisha, tumeitoa miili 20 kutoka katika eneo la ajali na walionusurika ni 10 wamekibizwa hospitali ya Mwingi Level Four Hospital,” amesema Kithei.

XS
SM
MD
LG