Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 05:25

COVID-19 : Kenya yachukua tahadhari zaidi dhidi ya aina mpya ya virusi


Ndege ya shirika la Kenya Airways ikiwa safarini.
Ndege ya shirika la Kenya Airways ikiwa safarini.

Kenya imepiga marufuku kusafiri kwenda Kusini mwa Afrika lakini Wizara ya Afya inasema itawachunguza kwa makini sana watu wanaowasili kutoka Afrika Kusini, Botswana na Hong Kong kubaini kama wana vriusi vipya vya Covid vilivyogunduliwa nchini Afrika Kusini

Kenya imepiga marufuku kusafiri kwenda Kusini mwa Afrika lakini Wizara ya Afya inasema itawachunguza kwa makini sana watu wanaowasili kutoka Afrika Kusini, Botswana na Hong Kong kubaini kama wana vriusi vipya vya Covid vilivyogunduliwa nchini Afrika Kusini.

Serikali ya Kenya imewaelekeza abiria wanaowasili kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kupima Covid kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini humo,

Afrika Kusini na Botswana zimeripoti virusi vipya katika nchi zao ambapo wanasayansi wanasema vinaambukiza kwa kasi kubwa na ni sugu kwa chanjo.

Mkurugenzi Mkuu wa Afya Kenya, Patrick Amoth ameiambia VOA kuwa nchi yake iko katika hali ya tahadhari kubwa sana kupambana na virusi hivi vipya.

“Tunafanya kazi kuhakikisha kwamba mfumo wetu wa ufuatiliaji ni wa hali ya juu na kuwaangalia haswa watu wanaokuja kutoka Afrika Kusini, Botswana na Hong Kong ili kuwaingiza katika mfumo imara wa ufuatiliaji. Tunasisitiza wawe wamepokea chanjo kamili kabla ya kuja nchini. Pia unatakiwa kuwa na majibu ya PCR kwamba huna virusi ambayo yametolewa ndani ya mud awa saa 96 kabla ya kuwasili nchini,” Amoth amesema.

Wiki hii, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisafiri kwenda Afrika Kusini, ambako alitia saini makubaliano ya kuboresha biashara na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.


Ili kupambana na kusambaa kwa virusi kwa watu, taifa hilo la Afrika Mashariki limezinduwa kampeni kabambe ya siku kumi kuanza Ijumaa, Kenya imefanikiwa kuwapatia chanjo takriban watu milioni 6.5.

Amoth anasema wana chanjo za kutosha kuwapatia watu wengi zaidi. “Ni sehemu ya mchakato wa chanjo unaoendelea na tunataka kuzidisha hali kulingana na matukio ambayo yanatokea huko Ulaya na kwingineko duniani. Kwahiyo ili kuhakikisha tunafikia watu wengi zaidi waliopata chanjo kwa lengo la kuwalinda watu nchini na hivi sasa tuna chanjo za kutosha kuongeza idadi ya watu kupatiwa chanjo,” ameongezea Amoth.

Amoth ameelezea imani yake kwamba wakenya wengi zaidi watapatiwa chanjo.

Kenya ina sera ya kutotoa huduma za serikali kwa watu ambao hawakupatiwa wakati ambapo pia wanawashawishi watu kujitokeza kupatiwa chanjo.

Kenya ina matumaini ya kuwapatia chanjo watu milioni 10 ifikapo mwisho wa mwaka huu.


XS
SM
MD
LG