Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:30

Afrika kusini ina dozi nyingi za chanjo dhidi ya Covid 19


Mtoto anayepewa chanjo dhidi ya virusi vya corona Diepsloot Township, karibu na Johannesburg, Oct. 21, 2021.
Mtoto anayepewa chanjo dhidi ya virusi vya corona Diepsloot Township, karibu na Johannesburg, Oct. 21, 2021.

Maafisa wa afya nchini Afrika kusini wamesema serikali imeomba makampuni ya Johnson and Johnson na Pfizer kuchelewesha utoaji wa chanjo za Covid 19 kwa sababu kwa sasa inazo nyingi kwenye maghala. Na hasa kutokana pia kusitasita kwa watu kuchukua chanjo jambo ambalo limedumuza zoezi la kuchanja watu.

Asilimia 35 ya wanainchi wa Afrika kusini wamekwisha pata chanjo kamili, ikiwa ni idadi kubwa kuliko katika mataifa mengine ya Afrika, lakini ni nusu ya wale serikali iliyolenga kuchanja kwa mwaka. Dozi laki 1 na elfu sita ndizo zilitolewa katika siku 15 zilizopita katika taifa hilo lenye watu millioni 60.

Mapema mwaka huu, kampeni ya kutoa chanjo ilikwamishwa na uhaba wa dozi za kutosha. Usambazaji wa dozi nyingine umecheleweshwa kutokana na kuwepo chanjo nyingi za kupita kiasi, na kuifanya nchi hiyo kuwa na chanjo nyingi zisizotumiwa katika bara ambalo watu wengi hawapati chanjo.

Nicholas Crisp, naibu mkurugenzi mkuu kwenye wizara ya afya ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba Afrika kusini ina dozi millioni 16.8 katika maghala na kusema kwamba uwasilishaji wa chanjo mpya umeahirishwa.

XS
SM
MD
LG