Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:45

Watu 20 wauawa kwa kupigwa risasi Afrika Kusini


Waopoaji wabeba mwili wa mmoja wa watu waliouawa kwenye moja ya mshambulizi ya risasi Afrika Kusini.
Waopoaji wabeba mwili wa mmoja wa watu waliouawa kwenye moja ya mshambulizi ya risasi Afrika Kusini.

Watu wasiopungua 20 waliuawa usiku wa kuamkia Jumapili katika mashambulzi ya bunduki katika baa mbili nchini Afrika Kusini, moja katika kitongoji karibu na Johannesburg, nyingine mashariki mwa nchi hiyo, polisi wamesema.

Katika kitongoji cha Soweto, watu 15 waliuawa walipokuwa wakijiburudisha usiku wa kuamkia Jumapili, wakati washambuliaji walipowasili, wakiwa wamebebwa teksi na kuanza kuwafyatulia risasi wateja kwa bunduki zenye nguvu nyingi, polisi wamesema.

Mamlaka katika mji wa mashariki wa Pietermaritzburg, jimbo la KwaZulu-Natal, zililiripoti kuwa watu wanne waliuawa na wanane kujeruhiwa wakiwa katika baa wakati wanaume wawili walipowafyatulia wateja risasi kiholela.

Huko Soweto, kitongoji kikubwa zaidi cha Johannesburg kusini magharibi mwa mji mkuu wa kiuchumi wa Afrika Kusini, polisi waliliambia shirika la habari la AFP kwamba walipofika kwenye eneo la tukio, watu 12 walikuwa wamekufa, wakiwa na majeraha ya risasi."

Watu 11 walipelekwa hospitalini, na watatu baadaye walikufa kutokana na majeraha yao.

Waliofariki, ambao ni pamoja na wanawake wawili, walikuwa na umri wa kati ya miaka 19 na 35, mkuu wa polisi wa mkoa Elias Mawela aliiambia AFP.

Hadi tulipokuwa tukitayarisha ripoti hii, hakukuwa na taarifa zozote kuhusu washambuliaji hao, na polisi walikuwa wakijaribu kubaini iwapo matukio hayo mawili yalikuwa na uhusiano wa moja kwa moja.

XS
SM
MD
LG