Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 16:10

Machar ashikiliwa Afrika Kusini


Riek Machar anayedaiwa kuzuiliwa Afrika Kusini

Shirika la habari la Reuters limesema vyanzo vya kidiplomasia na kisiasa vimesema Jumanne kuwa kiongozi wa uasi Sudan Kusini Riek Machar aliyetorokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi Agosti baada ya mapigano makali ameshikiliwa Afrika kusini ili kumzuia kuzua vurugu tena.

Zaidi ya watu milioni moja wametoroka Sudan Kusini tangu mapigano yalipoanza 2013 baada ya Rais Salva Kirr kutoka kabila la Dinka alipomfuta kazi Machar anayetoka kabila la Nuer kama makamu wake.

Kiongozi mmoja wa kisiasa mwenye ushawishi mkubwa kutoka Afrika kusini amesema Machar amezuiliwa nyumbani katika mji wa Pretoria wakati mienendo yake akifautiliwa kwa karibu na pia mawasiliano yake kwa njia ya simu kunaswa.

XS
SM
MD
LG