Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:00

Watu 15 wapigwa risasi katika maandamano Sudan


Maandamano Sudan : Watu 15 wapigwa risasi
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:37 0:00

Maandamano Sudan : Watu 15 wapigwa risasi

Mapigano ya mitaani yameutikisa tena mji mkuu wa Sudan Alhamisi siku moja baada ya vikosi vya usalama kuwaua kwa kuwapiga risasi waandamanaji 15 katika siku ya umwagaji damu mkubwa tangu jeshi lilipochukua madaraka Oktoba 25.

Mapigano ya mitaani yameutikisa tena mji mkuu wa Sudan Alhamisi siku moja baada ya vikosi vya usalama kuwaua kwa kuwapiga risasi waandamanaji 15 katika siku ya umwagaji damu mkubwa tangu jeshi lilipochukua madaraka Oktoba 25.

Polisi walifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji wengi wanaopinga mapinduzi ambao walikuwa wamekaa katika mitaa ya kaskazini mwa Khartoum usiku kucha, wakikabiliana na ukandamizaji mkali ambao umelaaniwa kimataifa, mashahidi walisema.

Polisi walibomoa vizuizi vya muda ambavyo waandamanaji walikuwa wameweka siku iliyotangulia.

Jenerali mkuu Abdel Fattah al-Burhan kiongozi mkuu wa Sudan tangu kuondolewa madarakani kwa rais wa muda mrefu Omar al-Bashir Aprili 2019 aliweka kizuizini uongozi wa kiraia na kutangaza hali ya hatari Oktoba 25.

Hatua hiyo iliinua mpito dhaifu wa Sudan kwa utawala kamili wa kiraia, na kuibua shutuma za kimataifa na msururu wa hatua za kuadhibu na kupunguzwa kwa misaada.

“Tunalaani ghasia dhidi ya waandamanaji wa amani na tunatoa wito wa kuheshimiwa na kulindwa haki za binadamu nchini Sudan," Ofisi ya Masuala ya afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema kwenye Twitter.

Burhan anasisitiza kuwa hatua ya jeshi "haikuwa mapinduzi" bali ni hatua ya "kurekebisha mwenendo wa mpito" kuelekea utawala wa kiraia.

Mamia ya watu wameingia mitaani jumatano kwenye mji wa khartoum na miji mingine lakini walikumbwa na ukandamizaji uliokuwa na mauaji tangu mapinduzi kutokea.

XS
SM
MD
LG