Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 09:14

Vuguvugu la demokrasia Sudan lakataa mazungumzo na jeshi


Muungano mkubwa wa ushirika wa kisiasa nchini Sudan, Jumatano umekataa mazungumzo yoyote ya makubaliano na jeshi.

Muungano huo unaendelea kushikilia msimamo wake katika mkutano wa kwanza na wanahabari toka kutokea mapinduzi Oktoba 25 yaliyofanywa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Katika taarifa iliyosomwa katika mkutano na wanahabari na msemaji wa umoja huo Alwathiq Elbereir, imeleza kwamba vuguvugu la na mabadiliko kulazimisha uhuru ambao ulitiwa saini mwaka 2019 na mabadilishano ya utawala na jeshi yaliyofikiwa baada ya kuondolewa kiongozi wa Sudan, Omar al-Bashir, limepinga mapinduzi na halijakutana na jeshi mpaka sasa.

Muungano huo unasema unamuunga mkono waziri mkuu aliyewekwa kizuizini Abdallah Hamdok, licha ya kutokutana naye na linataka kurejeshwa hali iliyokuwepo kabla ya mapinduzi.

XS
SM
MD
LG